Amekuwa mlinzi ADC na kuaminika na usalama wa mke wa Rais Janet Museveni ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Michezo nchini Uganda.
Safari ya Bainababo ya kufikia hadi kiwango chake cha sasa kikosini, ilianza alipojiunga na jeshi mwaka 1998 baada ya kupokea mafunzo ya msingi katika shule ya mafunzo ya Kabamba, iliyoko Mubende.
Charity Bainababo alijiunga na wanajeshi na kupokea mafunzo pamoja na Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mwanawe Yoweri Museveni.
Ikija kwenye historia ya wanawake waliofika kiwango cha juu kwenye jeshi la UPDF nchini Uganda, Brigedia Jenerali Charity Bainababo ni mmoja kati ya wanawake watatu wengine wakiwemo Luteni Jenerali Proscovia Nalweyiso na msemaji wa zamani wa UPDF Brigedia Flavia Byekwaso.
Mnamo Aprili 2022, Rais Yoweri Museveni alimpandisha madaraka Baibabo kutoka cheo cha Kanali alichopandishwa mwaka uliotangulia wa 2021 hadi daraja ya Brigedia Jenerali na pia kuteuliwa naibu kamanda wa kikosi maarufu cha SFC. Uteuzi huo umemfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuiamuru kitengo cha SFC.

Safari yake haikuwa rahisi kwani amepokea mafunzo katika viwango mbalimbali kati ya 1999 hadi 2017 kwani alihudhuria mafunzo ya kadeti, kozi ya makamanda na Chuo cha Kamandi na Wafanyakazi wa Kimaka.
Aidha, amehitimu Shahada ya Uzamili ya Ulinzi na Mafunzo ya Kimkakati katika Chuo Kikuu cha Makerere.

Charity pia ndiye kiongozi wa wabunge wa UPDF yani Dean.
Wakati huo huo, Bainababo ni kamanda wa polisi wa rais, ya kutoa ulinzi kwa mke wa rais na na watu wengine muhimu nchini Uganda.
Brigedia Jenerali Charity Bainababo, ameitumikia jeshi la Uganda kwa zaidi ya miaka 20 ambapo upaaji wake hadi ngazi za juu umemzolea heshima na kuwa kielelezo kwa wasichana na wanawake nchini Uganda.