Vijana na wanawake wa DRC wanahitaji usalama na maendelo na watazama hili kama kishawishi kikubwa kwao ili waweze kushiriki ipasavyo uchaguzi mkuu Disemba 20/ Picha : Reuters 

Na Hamisi Iddi Hamisi

Enzi na enzi nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikikabiliana na migogoro ya kiusalama katika baadhi ya maeneo. Kwani hivi sasa eneo la Mashariki mwa nchi halina amani kutokana na mapigano kati ya jehsi la DRC na kikundi cha waasi M23.

Ubadilishaji wa uongozi na harakati za kisiasa nchini humo unaweza kutazamwa kwa kupitia jicho la vijana na wanawake.

Sehemu yoyote ile takwa kuu la watu limekuwa ni usalama na amani. Vyivyo hivyo vijana na wanawake wa DRC wanahitaji usalama na maendelo na watazama hili kama kishawishi kikubwa kwao ili waweze kushiriki ipasavyo uchaguzi mkuu Disemba 20.

Delice Kawaya ni mfanyakazi kutoka mji wa Beni Mashariki mwa nchi, uliotikiswa kwa karibu miongo mitatu na migogoro ya usalama, hasa mashambulizi ya kundi la ADF. Akiwa na umri wa miaka 23, anataka kuona Rais wa zamani Felix Tshisekedi akiteuliwa tena kuiongoza DRC kwa miaka 5 mingine.

"Kulikuwa na kipindi ambacho watu wanaoishi pembezoni mwa mji walikuwa wakihamia kwa familia zinazowahifadhi,'' Kawaya aliambia TRT Afrika. ''Ilikuwa ngumu. Baadhi ya wasichana waliacha nyumba zao badala yake kwenda kwa wanaume, ambao wakati mwingine waliwanyanyasa kingono usiku kucha," Kawaya anasema.

Kawaya anaamini Rais aliyeko madarakani Felix Tshisekedi akipewa fursa ya pili itamruhusu kukamilisha mageuzi ndani ya jeshi lakini pia uundaji wa ajira na kuleta usalama nchini.

"Ikiwa tutawapigia kura watu wema hali yetu ya maisha itaboreka. Kwa upande mwingine, ikiwa tutawapigia kura watu wabaya mabadiliko yatakuwa mabaya," anasema Natalie Maliva na mwanaharakati ndani ya vuguvugu la kiraia ‘‘Pigana kwa ajili ya nchi yako’’ (LUCHA).

Kwa mujibu wa ripoti ya UN, wanawake wa DRC ndio wanawake wanaopata masaibu zaidi ya unyanyasaji duniani, hii ni kutokana na hali tete ya kivita iliyodumu kwa miaka mingi. / Picha : TRT Afrika 

Natalie anawahimiza vijana wenzake kufanya uchaguzi wa busara kwa sababu mustkabali wao unategemea hilo.

Ikiwa DRC ni nchi yenye rasimali nyingi zaidi kuliko nchi yoyote Afrika, Natalie anaamini wana uwezo wa kufanya kila kitu, kujenga mfumo wa viwanda, barabara, hospitali na mengine. Lakini yote haya yanawezekana ikiwa tu usalama utahakikishwa na watu wanaishi kwa amani.

Mbali na mtazamo kama wa Natalie kuna vijana kama Alice, mhitimu wa masuala ya kilimo na chakula lakini amewekeza kwenye mitindo. Anasema Disemba 20 ni siku kama siku zingine tu, katika juhudi za kutafuta fikra zake kuhusu uchaguzi jibu lake lilikuwa ni fupi ‘‘Sitapiga kura’’. Kwa mujibu wa Alice zoezi hili la kidemokrasia linaonekana kutoleta mabaliliko kwa idadi kubwa ya watu.

Nchini DRC kuna vyama vingi vya siasa huku vijana na wanawake wanajihusisha na harakati za vyama hivi kwa namna tofauti. Mifano mikubwa inayoweza kutolewa ni wagombea wanawake wawili kiti cha urais, Marie Josee Ifoku hii ikiwa ni mara yake ya pili na Joelle Bile wanatoa taswira kubwa kuhusu wanawake kujihusisha na siasa nchini DRC.

Uamuzi wao unaweka wazi nia yao ya kutaka kubadilisha mambo kadhaa kwa ajili ya jamii ya wakongomani. Na bila shaka wanataka kuwa sauti ya wanawake wengi ambao wanakumbana na mazingira magumu ikiwemo kukosa haki za kisheria, kunyanyaswa kingono na matatizo mengi yanayowakumba.

Kwa mujibu wa ripoti ya UN, wanawake wa DRC ndio wanawake wanaopata masaibu zaidi ya unyanyasaji duniani, hii ni kutokana na hali tete ya kivita iliyodumu kwa miaka mingi.

Swali la kujiuliza ni je, kutubutu huku kwa wanawake kutadumu kiasi gani na kutaleta athari gani kwa jamii yao? Kwani tayari mgombea Joelle Bile ametangaza Ijuma 5 Disemba kumuunga mkono rais Tshisekedi katika uchaguzi huu.

DRC ina watu zaidi ya milioni 100, asilimia 60 ya idadi hiyo ni vijana. / Picha : Reuters 

"Si bila sababu kwamba ninajiondoa tu, bali naweka macho yangu kwa Rais anayemaliza muda wake na mgombea wa nafasi yake mwenyewe. Uchaguzi huu unathibitishwa na nia yangu ya kuunganisha mafanikio, na kupendelea utetezi wa nchi yetu, huku nikihifadhi haki yetu na uhuru wa kitaifa," Joelle aliandika mtandao wa X.

Vishawishi vya kando kujiingiza kwenye siasa

Katika utetezi wa wanawake Denis Mukwege kitaaluma ni daktari aliyepigania maisha ya wanawake wengi waliobakwa tangu mwanzo wa vita vya pili vya Congo. Amekuwa sauti yao kwa kipindi kirefu mbali na kuwatibu tu, bila shaka hii imesukuma wanawake wengi kutaka kuingia kwenye siasa na kuweza kujihakikishia usalama wa Maisha yao.

Idadi inachangia vijana kujiihusisha na siasa.

Barani Afrika ikishika nafasi ya 3 kwa kuwa na idadi kubwa ya watu DRC ina watu zaidi ya milioni 100, asilimia 60 ya idadi hiyo ni vijana. Bila shaka hii ni sabbau tosha kwa vijana kutaka kujiongoza na kubdalisha mambo katika nchi yao.

TRT Afrika