P Diddy na Masaibu Yake
Je huu ndio mwisho wa P Diddy?
Tangu katikati ya Septemba jina la Puff Daddy au P Diddy limetawala vichwa vya habari kote duniani.
Lakini sio kwa wema.
Msanii huyo na gwiji wa muzuki wa rap Marekani anakabiliwa na shutuma nyingi ikiwemo ubakaji, unyanyasaji wa wasanii wengine, usaliti, na uhalifu wa kiuchumi.
P Diddy amezuiliwa katika gereza mjini New York na amenyimwa dhamana.