Utajiri wa Afrika: Hatari ya faru weupe kutoweka
Kenya inajivunia kuwa makazi ya faru wawili tu wa aina yake ambao wamebaki duniani.
Hawa ni faru weupe wa kaskazini au White Northern Rhinos.
Lakini pia kuna faru weupe wanaoitwa faru weupe wa Kusini au Southern rhinos.
Takwimu za mwaka 2023 zinaonyesha walikuwa 16,801.
Lakini faru hawa wako hatarini kwa sababu ya watu wanaosaka pembe zao.