| Swahili
ULIMWENGU
3 DK KUSOMA
Mahakama ya ICC yapendekeza kukamatwa kwa Netanyahu
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, ilisema kuwa inatafuta hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa ulinzi wa Israel na viongozi watatu wa kundi la Hamas.
Mahakama ya ICC yapendekeza kukamatwa kwa Netanyahu
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, ilisema kuwa inatafuta hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu / Picha: Reuters  / Others

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, ilisema kuwa inatafuta hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

"Kwa msingi wa ushahidi uliokusanywa na kuchunguzwa na Ofisi yangu, nina sababu za kuridhisha za kuamini kwamba Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, na Yoav Gallant, Waziri wa Ulinzi wa Israel, wanawajibika kwa uhalifu wa kivita na uhalifu wa kivita na ubinadamu uliofanywa katika eneo la Jimbo la Palestina (katika ukanda wa Gaza) kutoka 8 Oktoba 2023," Karima Khan, mwendesha mashtaka wa ICC amesema katika taarifa.

Mashtaka ambayo ameyaorodhesha dhidi ya Netanyahu ni pamoja na:

  • Njaa kwa raia kama njia ya vita kama uhalifu wa kivita

  • Kusababisha mateso makubwa kwa kudhamiria, au majeraha makubwa kwa mwili.

  • kutendewa kikatili kama uhalifu wa kivita kinyume na kifungu cha 8 (2)(c)(i); Kuua kwa kukusudia

  • Mauaji kama uhalifu wa kivita

  • Kuelekeza mashambulizi dhidi ya raia kwa kukusudia kama uhalifu wa kivita

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, pia inatafuta hati za kukamatwa kwa watu watatu, viongozi wa kikundi cha Hamas kwa madai ya majukumu yao katika mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 nchini Israel na kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

"Kwa msingi wa ushahidi uliokusanywa na kuchunguzwa na Ofisi yangu, nina sababu za kuridhisha za kuamini kwamba Yahya Sinwar (Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (“Hamas”) katika Ukanda wa Gaza), Mohammed Diab Ibrahim Al - Masri anayejulikana zaidi kama Deif (Kamanda Mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, linalojulikana kama Brigedi za Al-Qassam)," taarifa hiyo imeongezea.

"Na Ismail Haniye (Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas) wanawajibika kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu unaofanywa katika eneo la Israeli na Jimbo la Palestina (katika ukanda wa Gaza) kutoka angalau 7 Oktoba 2023," imeongezea.

Mashataka ambayo yapo dhidi yao ni pamoja na:

  • Mauaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu

  • Kuchukua mateka kama uhalifu wa kivita

  • Ubakaji na vitendo vyengine vya unyanyasaji wa kijinsia

  • Kuwatesa watu

  • Vitendo vya kikatili

"Ofisi yangu inakubali kwamba uhalifu wa kivita unaodaiwa katika maombi haya ulitekelezwa katika muktadha wa mzozo wa kimataifa wa silaha kati ya Israel na Palestina, na mzozo wa silaha usio wa kimataifa kati ya Israel na Hamas unaoendana sambamba," ICC imesema.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Rais wa Brazil Lula da Silva apata ushindi wa kihistoria wa muhula wa 4 dhidi ya Flavio Bolsonaro
Maandamano Ufaransa yakigeuka kuwa ya vurugu, huku maelfu wakikamatwa katika miji tofauti
Maelfu ya Waisraeli waandamana Tel Aviv kudai kukomeshwa kwa enzi ya Netanyahu kabla uchaguzi
Papa Leo XIV ahairisha ziara ya Assisi kwa ushauri wa madaktari
Marekani yawaagiza wanadiplomasia wake na familia zao kuondoka nchi za Ghuba
Trump asema Marekani haijadiliani na Iran, aashiria kuwashughulikia 'hivi karibuni'
Iran kuzindua bomu lake kubwa zaidi “father of all bombs”
Uturuki, Qatar, Indonesia na Pakistan zasaini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi ya 'Badr'
Uingereza kupeleka ndege za kivita Saudi Arabia kuilinda dhidi ya mashambulizi ya Wahouthi
Makamu wa Rais wa Ufilipino, Sara Duterte apinga kung’olewa madarakani
Dereva amgonga mbunge wa Australia, amwacha mahututi
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth akutana na Netanyahu katika ziara ya kushtukiza Israel
Shambulio la Wahouthi lauwa watu kadhaa katika kituo cha mafunzo ya kijeshi Yemen
Machafuko ya Ulaya yafichua madhila ya uchumi, ufisadi na mzigo wa madeni
Mahakama Marekani yatoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa Cuba Raul Castro
Maandamano nchini Albania yaingia siku ya sita huku Waziri Mkuu Rama akikataa wito wa kujiuzulu
Wahouthi washambulia Ikulu ya Yemen kwa makombora, 5 wauawa
Saudi Arabia yazuia kombora katika anga ya mji wa Madinah
Urusi yaituhumu Ukraine kwa kushambulia mitambo yake ya kusafishia mafuta
Ujerumani yapiga marufuku matumizi ya pombe kwenye vituo vya treni