Uturuki miongoni mwa mataifa yaliyo katika makubaliano ya kulinda bahari

Mkataba wa kulinda bahari katika maeneo ya kimataifa ni mwanzo mpya unaoweka utaratibu wa kuratibu shughuli za baharini, ikiwemo marufuku ya uvuvi, katika maeneo yaliyotengwa kama hifadhi.

By
Bayram Ozturk, mkuu wa Taasisi ya Uturuki ya Utafiti wa Baharini (TUDAV), alieleza makubaliano kuwa mwanzo mpya katika kulinda bahari duniani. /AA

Mkataba wa kulinda bahari, unaojulikana kama makubaliano ya BBNJ, utaanza kutekelezwa Jumamosi tarehe 17, baada ya kuidhinishwa na mataifa 60, kuashiria hatua muhimu ya kulinda viumbe katika bahari za kimataifa.

Makubaliano hayo ambayo yalipitishwa na Umoja wa Mataifa 2023, yanaweka utaratibu wa kisheria ya kuwa na maeneo yanayolindwa baharini na kuhitaji kufanyike tathmini ya mazingira kwa shughuli za baharini ambazo huenda zikaleta madhara kwa viumbe kwenye maji.

Uturuki ni sehemu ya makubaliano

Kote duniani maeneo 16,600 ya baharini yanayolindwa ni asilimia 9.6 ya bahari ulimwenguni, lakini asilimia 3.2 ndiyo yanayolindwa kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuratibu shughuli za uvuvi, hii ni kulingana na Taasisi ya Kulinda maeneo ya Bahari ya Marine Protection Atlas.

Akizungumza na Anadolu, Bayram Ozturk, mkuu wa Taasisi ya Uturuki kuhusu Utafiti wa Baharini (TUDAV), alieleza makubaliano hayo kuwa mwanzo mpya katika kulinda bahari duniani.

Alisisitiza kuwa maeneo yanayolindwa baharini hayapigi marufuku kote katika bahari ya kimataifa, lakini inatengeneza utaratibu wa kuratibu shughuli, ikiwemo kupiga marufuku katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi.

Utekelezaji kikamilifu wa makubaliano ya BBNJ kutasaidia kulinda viumbe vya baharini na kuleta usawa katika kuratibu masuala ya bahari, alisema.

Levent Bilgili wa Kitivo cha Mafunzo ya Bahari katika Chuo Kikuu cha Bursa anasema mkataba huo utahitaji meli za mataifa yanayoshiriki katika kulinda na kufanya operesheni kwenye bahari za kimataifa kutimiza viwango vya hali ya juu na kulinda mazingira.

Kongamano la Umoja wa Mataifa la Tabianchi (COP31), lililopangwa kufanyika mwezi Novemba, linatarajiwa kufanyika mjini Antalya, katika pwani ya Uturuki ya Mediterani, huku mkutano wa viongozi ukitarajiwa kufanyika jijini Istanbul.

Kama moja ya mataifa yaliyo kwenye makubaliano ya BBNJ, kushiriki kwa Uturuki kikamilifu kunaimarisha nafasi yake kama wenyeji wa COP31, ambapo masuala yanayohusiana na bahari na tabianchi yanatarajiwa kuwa kwenye agenda, Bilgili ameiambia Anadolu.