FIFA yafikiria kuiondolea Urusi adhabu ya kushiriki michuano ya kimataifa
Timu za taifa za Urusi zilisimamishwa kushiriki michuano iliyoandaliwa na FIFA na UEFA, mwezi Februari 2022, baada ya taifa hilo kuivamia Ukraine.
Rais wa FIFA Gianni Infantino akiwa pamoja na Rais Vladimir Putin wa Urusi./Picha:Wengine
Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino amesema kuwa shirikisho hilo linafikiria kuiondolea Urusi adhabu ya kushiriki michuano ya kimataifa.
“Adhabu hii maana yoyote, kimsingi imezidi kupandikiza chuki tu,” alisema Infantino.
Hata hivyo, kwa upande wake, Waziri wa michezo wa Ukraine, Matvii Bidnyi ameielezea kauli ya Infantino kuwa imekosa uwajibikaji.
Timu za taifa za Urusi zilisimamishwa kushiriki michuano iliyoandaliwa na FIFA na UEFA, mwezi Februari 2022, baada ya taifa hilo kuivamia Ukraine.