Rais Erdogan wa Uturuki alaani shambulizi dhidi ya Azerbaijan

Kulingana na Wizara ya Afya ya Azerbaijan, watu wanne wamejeruhiwa kufuatia shambulio hilo.

By
Erdogan alilaani shambulizi hilo, akimtumia kiongozi mwenzake salamu za rambirambi na watu wote Azerbaijan./Picha:AAi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Azerbaijan, Ilham Aliyev wamefanya mazungumzo ya simu, wakijadiliana shambulizi la ndege nyuki katika eneo la Nakhchivan, na kujeruhi watu wanne.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika siku ya Alhamisi, Erdogan alilaani shambulizi hilo, akimtumia kiongozi mwenzake salamu za rambirambi na watu wote Azerbaijan, kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Mapema siku hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje pia ilitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo.

“Matukio kama haya ni lazima yakomeshwe mara moja,” ilisema Wizara hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Uturuki itaendelea kusimama pamoja na Azerbaijan.

Mapema Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Azerbaijan alisema kuwa eneo la nchi hiyo lilishambuliwa na ndege nyuki za Iran, huku moja likilenga sehemu ya jengo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nakhchivan International Airport, na lingine likidondekea karibu na shule katika kijiji cha Shakarabad.

“Tunalaani vikali mashambulizi hayo kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo yamesababisha uharibifu na watu wawili kujeruhiwa,” ilisema wizara hiyo.

Hata hivyo, mamlaka za Iran hazijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.

Mazungumzo na Waziri Mkuu wa Malaysia

Mapema Alhamisi, Erdogan alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim, wawili hao wakijadiliana masuala ya kikanda na kiulimwengu kwa njia ya simu.

Kulingana na Erdogan, uhusiano kati ya Uturuki na Malaysia unaendelea vyema katika nyanja zote.

Erdogan alisema kuwa, Uturuki inafuatilia kwa karibu yanayoendelea katika kanda hiyo, akisisitiza mgogoro huo utaleta hali mbaya zaidi katika eneo hilo.

Pia, aliongeza kuwa Uturuki inaendeleza jitihada za kidiplomasia na amani.