Marekani na Iran zapiga hatua kubwa za makubaliano: Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa kuna hatua kubwa za makubaliano zilizofikiwa katika mazungumzo kati ya Marekani na Iran.

By Mustafa Abdulkadir
Rais Trump amesema majadiliano na Iran yataendelea kwa wiki nzima, kuashiria uwezekano wa suluhu la kidiplomasia. /AP / AP

Kulingana na Rais wa Marekani, Donald Trump, mazungumzo hayo yanapaswa kuifanya Iran kuachana kabisa na mpango wake wa nyuklia pamoja na akiba yake ya urani iliyorutubishwa.

Donald Trump, ameeleza kuwa ‘’mabadiliko ya utawala’’ yatafanyika nchini Iran, na kuonya kuwa ikiwa mazungumzo na viongozi wa Iran waliowasiliana na Marekani hayatofanikiwa, mashambulizi ya mabomu yataendelea.

Aidha, amesema kuwa pande zote mbili—Marekani na Iran—zina nia ya kufikia makubaliano, na kwamba tayari zimefanya mazungumzo yenye uzito mkubwa. Na kwamba wajumbe wa Marekani wamekuwa wakikutana na kiongozi wa Iran “anayeheshimika”.

Ameongeza kuwa iwapo makubaliano yatafikiwa, Marekani itachukua hatua ya kudhibiti urani iliyorutubishwa ya Iran, ambayo ni nyenzo muhimu katika mpango wa nyuklia.

Hata hivyo, Rais Trump amesema hawezi kutoa uhakika wa kufikiwa kwa makubaliano hayo, akibainisha kuwa makubaliano yoyote yatakuwa mwanzo mzuri kwa Iran na kwa eneo lote kwa ujumla.