| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Trump: Vita dhidi ya Iran vilichangia kushindwa kwa chama cha Republican katika uchaguzi
"Nadhani sehemu ya sababu ilikuwa ni Iran, lakini wakati huohuo, watu walielewa umuhimu wa hatua nilizochukua kuhusu Iran," alisema Trump.
Trump: Vita dhidi ya Iran vilichangia kushindwa kwa chama cha Republican katika uchaguzi
Trump alisema kuwa chama cha Democratic kitapeleka kwake miswada ambayo haina mantiki, lakini ameapa kuipinga kwa kutumia mamlaka yake ya urais. /

Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kuwa vita dhidi ya Iran vimechangia kushindwa kwa wagombea wa Chama cha Republican katika uchaguzi wa nusu muhula uliofanyika Jumanne.

Hayo yanajiri huku Chama cha Democratic kikijiandaa kuchukua udhibiti wa Baraza la Wawakilishi na Seneti, hatua inayoweza kukwamisha baadhi ya ajenda zake za kisiasa na kisheria.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox News, Trump alisema kuwa wabunge wa chama cha Democratic watapeleka mezani kwake miswada ambayo anaiona kuwa haina mantiki, lakini ameapa kuipinga kwa kutumia mamlaka yake ya urais.

"Wataleta miswada ambayo haina mantiki, nami nitapinga kuipitisha. Baada ya miezi kadhaa ya mimi kuipinga miswada hiyo, watapiga simu na kuuliza, 'Tunawezaje kufanikisha mambo haya?' Ndipo tutakapokaa pamoja na kutafuta namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano," alisema Trump.

Trump pia alikiri kuwa vita dhidi ya Iran vilikuwa miongoni mwa mambo yaliyoathiri wagombea wa Republican katika uchaguzi huo, licha ya kudai kuwa wapiga kura waliunga mkono namna alivyosimamia suala hilo.

"Nadhani sehemu ya sababu ilikuwa ni Iran, lakini wakati huohuo, watu walielewa umuhimu wa hatua nilizochukua kuhusu Iran," alisema.

CHANZO:TRT World and Agencies