Orodha ya timu 10 za Afrika zitakazoshiriki Kombe la Dunia 2026
Timu kumi za mataifa ya Afrika zitashiriki katika fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiwa ni uwakilishi mkubwa zaidi kutoka bara la Afrika.
Timu kumi za mataifa ya Afrika zitashiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiwa ni idadi kubwa zaidi kutoka kwenye bara hilo.
Timu hizo ni Morocco, Tunisia, Misri, Algeria, Senegal, Côte d'Ivoire, Ghana, Cape Verde, Afrika Kusini, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mashindano ya Kombe la Dunia 2026 yatakuwa na wenyeji mwenza Marekani, Mexico, na Canada kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, 2026.
Timu za Kombe la Dunia 2026 ziliongezwa kutoka 32 hadi 48, na mchakato wa kuwania nafasi za kufuzu ulibadilishwa.
Huku timu tisa kutoka Afrika zikipata nafasi za moja kwa moja, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa ya kumi kufuzu baada ya kuishinda Jamaica 1-0 katika mechi za mtoano za mabara tofauti siku ya Jumanne.