MICHEZO
1 dk kusoma
Algeria yafuzu kwa Kombe la Dunia 2026
Algeria imefuzu kwa Kombe la Dunia siku ya Alhamisi, ikiwa ni timu ya nne kutoka Afrika kupata nafasi hiyo kwa mashindano yatakayofanyika Marekani Kaskazini mwakani, baada ya kuwafunga Somalia 3-0.
Algeria yafuzu kwa Kombe la Dunia 2026
Algeria sasa ni timu ya nne kutoka Afrika kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026, baada ya Misri, Tunisia na Morocco. / Picha: Reuters
tokea masaa 9

Algeria imefuzu kwa Kombe la Dunia siku ya Alhamisi, ikiwa ni timu ya nne kujikatia tiketi kwa mashindano hayo yatakayofanyika Marekani Kaskazini baada ya kuifunga Somalia 3-0.

Mohamed Amoura amefunga magoli mawili – na kufikisha idadi yake ya magoli katika kuwania kufuzu hadi nane – na nahodha Riyad Mahrez pia alifunga.

Ushindi huu wa Algeria unawafanya kuwa na jumla ya alama 22 ikiwa bado wamebakisha mechi moja kucheza katika kundi G. Itakuwa fainali ya tano ya Kombe la Dunia lakini ya kwanza tangu mashindano yaliyochezwa Brazil 2014.

Timu itakayoibuka wa kwanza katika kila kundi kwa makundi tisa ya Afrika inafuzu moja kwa moja kwa mashindano hayo yatakayochezwa Canada, Mexico na Marekani, na Algeria inaungana na Morocco, Tunisia na Misri ambao pia tayari wamefuzu.

CHANZO:TRT Afrika Swahili