Mreno Carlos Queiroz kuifundisha ‘Black Stars’ ya Ghana

Queiroz anaripotiwa kupokea kitita cha Dola 90,000 kama mshahara wake kwa mwezi katika kazi yake hiyo mpya.

By
Queiroz anaripotiwa kupokea kitita cha Dola 90,000 kama mshahara wake kwa mwezi katika kazi yake hiyo mpya./Picha:Reuters

Kocha wa zamani wa klabu za Manchester United na Real Madrid Carlos Queiroz, ametwaa mikoba ya kuifundisha timu ya taifa Ghana ambayo itashiriki michuano ya Kombe la Dunia miezi miwili ijayo.

Queiroz, ambaye aliwahi pia kuzifundisha timu za Ureno, Afrika Kusini na Iran, amepewa mkataba wa miezi minne wa kuifundisha ‘Black Stars’ kwa masharti ya kuendelea kubakia Ghana iwapo atafanikiwa kuifikisha timu huyo kwenye hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo mikubwa duniani.

Queiroz anaripotiwa kupokea kitita cha Dola 90,000 kama mshahara wake kwa mwezi katika kazi yake hiyo mpya.

Anatarajiwa kuwasili ndani ya kikosi cha Ghana akiwa na benchi la ufundi lenye jumla ya watu watano.