| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Netanyahu ahairisha ziara yake ya Marekani
Ziara ya Netanyahu nchini Marekani, ilihusisha kukutana na Rais Donald Trump na pia kuhudhuria mazishi ya Seneta Lindsey Graham.
Netanyahu ahairisha ziara yake ya Marekani
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu./Picha:Reuters

Ziara ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuelekea nchini Marekani, sasa imeahirishwa.

Katika taarifa yake iliyotolewa Julai 16, 2026, ofisi ya kiongozi huyo, ilisema kuwa ziara hiyo iliyokuwa ifanyike wiki ijayo, imehairishwa mpaka mwisho wa mwezi wa saba.

Ziara ya Netanyahu nchini Marekani, ilihusisha kukutana na Rais Donald Trump na pia kuhudhuria mazishi ya Seneta Lindsey Graham.

"Hivyo basi, waziri mkuu hatosafiri kuelekea nchini Marekani kama ilivyoarifiwa hapo awali," taarifa hiyo ilisema.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo uhusiano wa Marekani na Israel, umeingia dosari kutokana na sera za kikanda.

Katika siku za karibuni, Trump ameitaka Israel ijiondoe kutoka Lebanon na Syria, hatua ambayo imepingwa na Israel.

CHANZO:Anadolu Agency