| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Osimhen aipeleka Galatasaray 16 bora ya UEFA
Nyota huyo wa Nigeria alifunga bao muhimu katika dakika za majeruhi za muda wa nyongeza, na kuwapa nafasi ya Galatasaray nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Osimhen aipeleka Galatasaray 16 bora ya UEFA
Nyota wa Nigeria, Victor Osimhen./Picha:Reuters
tokea masaa 11

Victor Osimhen aliifungua Galatasaray bao muhimu usiku wa Jumatano, na kumfanya awe mfungaji bora wa muda wote kutoka  nje ya Ulaya kufanya hivyo kwenye mashindano ya UEFA, akiwa ndani ya jezi ya Galatasaray.

Nyota huyo wa Nigeria alifunga bao muhimu katika dakika za majeruhi za muda wa nyongeza, na kuwapa nafasi ya Galatasaray nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Licha ya kupoteza kwa mabao 3-2 jijini Turin, bado Galatasaray, inasonga mbele kwenye michuano hiyop, kufuatia karamu yao ya mabao waliyoipata katika mchezo wa kwanza.

Juventus ilianza kufungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Manuel Locatelli kwa njia ya tuta, baada ya Lucas Torreira kumfanyia madhambi Khephren Thuram.

Wenyeji hao, walilazimika kumaliza mchezo wakiwa 10 uwanjani baada ya kipindi cha pili, baada ya Lloyd Kelly kuoneshwa kadi nyekundu.