Droni iliyotengenezwa Urusi yaanguka kaskazini magharibi mwa Uturuki: wizara

Tukio hilo linajiri baada ya Uturuki kuidungua ndege isiyokuwa na rubani siku ya Jumatatu ambayo "ilipoteza muelekeo" wakati ikikaribia anga yake kutoka Bahari Nyeusi.

By
Inaaminika kuwa ndege isiyokuwa na rubani ya Urusi. / TRT Arabi / TRT ARABI

Ndege isiyokuwa na rubani aina ya UAV inayoaminika kutengenezwa Urusi imepatikana katika eneo la Cubuklubala wilaya ya Izmit kaskazini magharibi mwa mkoa wa Uturuki wa Kocaeli, kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki.

Katika taarifa siku ya Ijumaa, wizara ilisema UAV hiyo inasemekana kuwa muundo wa Orlan-10, ambayo hutumiwa zaidi kwa sababu za tathmini kwanza.

Uchunguzi kuhusu matukio hayo yanaendelea, iliongeza.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti ndege hiyo isiyokuwa na rubani iliharibika ilipoanguka.

Tukio hilo linakuja baada ya Uturuki kudungua droni siku ya Jumatatu ambayo "ilipoteza muelekeo" wakati ikikaribia anga yake kutoka Bahari Nyeusi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonya dhidi ya Bahari Nyeusi kuwa "eneo la mapigano" kati ya Urusi na Ukraine, kufuatia mashambulizi katika wiki za hivi karibuni dhidi ya meli katika eneo hilo.

Meli ya Uturuki iliharibiwa wiki iliopita kutokana na shambulio la angani la Urusi karibu na mji wa bandari wa Ukraine wa Odessa, saa chache baada ya Erdogan kuzungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin pembeni mwa mkutano nchini Turkmenistan.