| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki azungumza na wenzake wa Iran na Pakistan
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki inasema mazungumzo hayo yaliangazia yanayoendelea katika mchakato wa majadiliano kati ya Iran na Marekani.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki azungumza na wenzake wa Iran na Pakistan
Mazungumzo yanafuatia makubaliano ya usitishaji mapigano kwa wiki mbili, yaliyoratibiwa na Pakistan Aprili 8. / AA

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amefanya mazungumzo kwa njia ya simu katika nyakati tofauti na wenzake wa Iran na Pakistan, Wizara ya Mambo ya Nje imesema.

Mazungumzo hayo ya Jumamosi kati ya Hakan Fidan, Abbas Araghchi na Ishaq Dar yaliangazia yanayojiri katika mchakato wa majadiliano kati ya Iran na Marekani, kulingana na wizara hiyo.

Duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran ilifanyika mjini Islamabad wiki mbili zilizopita lakini hakuna muafaka uliofikiwa kumaliza mzozo ulioanza Februari 28 na kuenea kote Mashariki ya Kati.

Mazungumzo hayo yanafuatia makubaliano ya usitishaji wa mapigano kwa wiki mbili yaliyoratibiwa na Pakistan Aprili 8, ambapo baadaye Rais wa Marekani Trump aliongeza muda huo.

CHANZO:AA