Benki Kuu ya Sudan yaondoa marufuku ya dhahabu kutouzwa nje ya nchi

Chini ya marufuku iliyowekwa hapo awali Benki kuu ya Sudan iliwajibisha wauzaji dhahabu nje ya nchi kuzingatia udhibiti uliotolewa na Wizara ya Viwanda, Wizara ya Madini, Shirika la Viwango na Hali ya hewa la Sudan, na Kampuni ya Sudan Gold Refinery.

By
Sudan inasema dhahabu mingi inapotea kwa biashara ya magendo

Benki Kuu ya Sudan siku ya Jumatano iliamua kuruhusu makampuni ya kuuza dhahabu nje ya nchi, baada ya kupiga marufuku hatua hiyo Septemba 2025.

Uamuzi wa Benki Kuu, uliotolewa mnamo Septemba 15, ulisababisha mzozo kati ya taasisi za serikali na wauzaji bidhaa nje ambao waliukanusha.

Benki hiyo ilisema katika taarifa kwamba sasa "inaruhusu usafirishaji wa dhahabu nje ya nchi na mtu yeyote baada ya kutimiza taratibu za usafirishaji, mradi inauzwa nje kulingana na bei ya soko la kimataifa."

Ilibainisha kuwa malipo ya mauzo ya dhahabu lazima yakusanywe kupitia malipo ya awali au barua za mkopo, ambayo haitakiwi kujumuisha masharti yanayohusiana na kubadilisha bidhaa nje ya nchi, na thamani ya mapato ya mauzo ya nje kurejeshwa ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya usafirishaji.

Benki Kuu iliruhusu wasafirishaji wa dhahabu kutumia mapato yao ya mauzo ya nje na pia iliruhusu kuuzwa kwa benki yoyote au Benki Kuu.

Uzalishaji wa dhahabu wa Sudan katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali kuu ulifikia tani 53 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu, wakati mapato ya mauzo ya nje yalikuwa yasiyopungua dola milioni 909, na kusababisha vyombo kadhaa kuchunguza tofauti za bei.

Marukufu ilihusisha nini?

Chini ya marufuku iliyowekwa hapo awali Benki kuu ya Sudan iliwajibisha wauzaji dhahabu nje ya nchi kuzingatia udhibiti uliotolewa na Wizara ya Viwanda, Wizara ya Madini, Shirika la Viwango na Hali ya hewa la Sudan, na Kampuni ya Sudan Gold Refinery.

Ilifafanua kuwa kiwango cha chini cha kuidhinisha makubaliano ya mauzo ya nje ni kilo 10 za dhahabu.

Pia ilipiga marufuku mashirika ya serikali na wageni, wawe watu binafsi au makampuni, kusafirisha nje ya nchi madini hayo ya thamani, isipokuwa makampuni yanayotimiza masharti.

Waraka huo ulipunguza jukumu la Benki Kuu katika ununuzi wa dhahabu ili kuimarisha akiba ya bidhaa.

Dhahabu nyingi nchini Sudan huzalishwa na uchimbaji mdogo mdogo wa madini, ambao huajiri takriban watu milioni mbili.

Wakati huo huo, kampuni nyingi zinategemea kuchimba dhahabu kutoka kwa madini ya asili, inayojulikana kama "Karta," ambayo huchakatwa kwa dutu za kemikali kama vile sianidi.

Nyingi ya dhahabu inayozalishwa husafirishwa kwa njia ya magendo hadi nchi kadhaa,

Serikali ya Sudan sasa inashtumu mnunuzi mkubwa wa dhahabu Imarati (UAE) kwa kuhusika na magendo ya dhahabu na hivyo kuinyima Sudan fedha muhimu za kigeni zinazohitajika kufadhili uagizaji wa bidhaa, hasa unga wa ngano na mafuta.