Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atakutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas siku ya Jumatano wakati wa ziara rasmi ya kiongozi huyo wa Palestina nchini Uturuki; taarifa hii imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha nchi hiyo siku ya Jumanne.
Abbas anatarajiwa kuwasili katika mji mkuu, Ankara, siku ya Jumanne kwa ziara rasmi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Erdogan, kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Uturuki, Burhanettin Duran, kupitia mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal.
Katika mkutano wao, Erdogan na Abbas watajadili yanayojiri nchini Palestina na katika kanda, uhusiano wa mataifa mawili, Duran ameongeza.
ZILIZOPENDEKEZWA
CHANZO:AA






















