Wapishi wa vyakula vya msaada Sudan walengwa na RSF: UN yatahadharisha

Umoja wa Mataifa umesema mpaka sasa haijabainika kwa nini wafanyakazi wa kutoa msaada wa chakula wanalengwa.

By
ula na mahitaji ya msingi yakipungua. Msaada kupitia vyakula vya vinavyopikwa kwa jumuia umekuwa muhimu kwa maisha ya watu / Reuters

Wafanyakazi wa misaada ya chakula wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara katika mgogoro kati ya Jeshi la Sudan and Vikosi vya RSF, vita ambavyo vimeenea nchi nzima, na kusababisha mauaji ya maelfu, wengine wakikosa makazi, mlipuko wa magonjwa, na uhaba wa chakula, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Dan Teng’o, mkuu wa mawasiliano wa UN, Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, amesema haiko wazi iwapo wafanyakazi wa msaada wa chakula wanalengwa kwa sababu ya kazi yao ya kibinadamu au kwa sababu wanaonekana kama wanaegemea upande mmoja wa mgogoro.

“Kudorora kwa hali ya usalama kumeathiri jamii, ikiwemo wanaojitolea kupika vyakula kwa jamii," amesema Teng'o.

Wanaharakati wanasema wapishi wanaonekana sana katika jamii, hivyo kushambuliwa kwa urahisi na makundi yenye silaha.

Ulipaji wa fidia unaanzia $2,000 hadi $5,000 — mara nyingi ikiongezeka pindi familia zinapoanza kufanya malipo.

Kuwakimbia RSF

Farouk Abkar, 60, kutoka Al Fasher, amekuwa akisambaza magunia ya chakula kwa muda wa mwaka mzima katika kambi ya Zamzam, takriban kilomita 15 kusini mwa mjini.

Ameiambia Associated Press (AP) kwamba alisalimika na mashambulizi la ndege zisizo na rubani na anakumbuka siku sehemu ya jimbo ilivyoshambuliwa na wapiganaji wa RSF.

Abkar aliondoka Al Fasher na binti yake usiku, na kutembea kwa siku kumi mfululizo.

Enas Arbab, mfanyakazi mwengine wa misaada, amesema alikimbia jimbo la magharibi mwa Sudan Darfur baada ya mji wake kuwa chini ya udhibiti wa wapiganaji.

Alitoroka yeye na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja, huku kumbukumbu za baba yake aliyeuliwa, kwa sababu alikuwa akifanya kazi jikoni na kuwahudumia waliokosa makazi.

RSF ambayo imekuwa katika mgogoro na Jeshi la Sudan tangu Aprili 2023, awali iliuzingira mji wa Al Fasher.

Maafisa wa U.N. wanasema maelfu ya raia waliuawa pindi RSF ilipochukua eneo hilo Oktoba mwaka jana.

Ni asilimia 40 tu ya wakazi wa Al Fasher 260,000 ambao waliweza kukimbia machafuko, huku maelfu wakijeruhiwa, kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa.

Hatma ya waliobaki mpaka sasa haijulikana.

Darfur na maeneo mengine ambapo mapigano makali yanaendelea, ukame umeenea huku chakula na mahitaji ya msingi yakipungua.

Msaada kupitia vyakula vya vinavyopikwa kwa jumuia umekuwa muhimu kwa maisha ya watu, lakini wengi wa waliojitolea wametekwa, wameibiwa, wamefungwa, wamepigwa, au kuuawa, kwa mujibu wa UN.