| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Uganda yatia saini muswada wa kuzuia uingiliaji wa mataifa ya kigeni
Adhabu ya kukiuka ni hadi kifungo cha miaka 10 gerezani na faini kubwa.
Uganda yatia saini muswada wa kuzuia uingiliaji wa mataifa ya kigeni
Rais Yoweri Museveni alieleza nia ya Muswada huo katika taarifa ya kurasa nne na kuiweka kwa umma Aprili 30 2026. / Reuters

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini kuwa sheria hatua za kukabiliana na uingiliaji wa mataifa ya nje katika masuala ya nchi yake, licha ya hofu kutoka kwa baadhi ya taasisi kama vile benki kuu.

Museveni mwenye umri wa miaka 81, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, kwa miaka kadhaa amekuwa akilalamika kuhusu uingiliaji wa masuala ya Uganda kutoka kwa mataifa ya nje.

Museveni ametia saini sheria hiyo, ofisi yake ilisema katika taarifa Jumapili jioni.

Muswada wa "Kulinda Uhuru", ulioidhinishwa mwezi huu, unafanya kuwa kosa la jinai kupigia chapuo "maslahi ya raia wa kigeni dhidi ya maslahi ya Uganda" na inahitaji maafisa wa kigeni kujisajili.

Marufuku ya serikali

Pia inapiga marufuku yeyote anayefanya kazi kwa niaba ya maslahi ya mataifa ya nje kutengeneza au kuimarisha sera zao bila idhini ya serikali.

Kupitia taarifa, Ofisi ya rais, inasema sheria hiyo imeundwa ili kulinda uhuru wa mamlaka ya Uganda “bila kuingiliwa na mataifa ya nje,” na kupiga marufuku “maafisa” kujihusisha na masuala ya kisiasa yanayohusishwa na maslahi ya nchi za nje.

Adhabu ya kukiuka ni hadi kifungo cha miaka 10 jela na faini kubwa.

Gavana wa Benki Kuu ​Michael Atingi-Ego ameonya kuwa sheria hiyo itasababisha kusitishwa kwa fedha zinazoingia nchini Uganda na kupunguza akiba ya fedha za kigeni.

CHANZO:TRT Afrika Swahili