| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
DR Congo yakana kutoa rasilimali zake za madini katika makubaliano ya amani ya Trump
Makubaliano hayo yanawezesha upatikanaji wa shaba, cobalt, coltan na Lithium kwa kampuni za Marekani, lakini Waziri wa Madini wa Congo amesema nchi yake haijauza chochote mpaka sasa.
DR Congo yakana kutoa rasilimali zake za madini katika makubaliano ya amani ya Trump
DRC ina utajiri mkubwa wa rasilimali ambao bado haujaendelezwa. / Reuters
12 Februari 2026

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo "haijauza" rasilimali zake za madini kwa Marekani kupitia makubaliano yanayoipa Marekani uwezo wa kufikia akiba yake ya madini, amesema Waziri wa Madini wa nchi hiyo.

Makubaliano yaliyosainiwa mwezi Disemba yanafungua mlango kwa makampuni ya Marekani kuweza kufikia shaba, cobalt, coltan na lithium, pamoja na makubaliano ya amani yenye lengo la kusitisha mgogoro wa muda mrefu mashariki mwa DRC.

Rais wa Marekani Donald Trump amesifu makubaliano hayo kama ukurasa mpya wa furaha na ushirikiano ambao ungeleta amani na maendeleo katika eneo hilo.

"DRC haijauza chochote kabisa. DRC haijauza chochote kabisa," amesema Waziri Louis Watum pembezoni mwa mkutano wa madini wa African Mining Indaba Conference unaoendelea Cape Town, Afrika Kusini.

Mazungumzo ya Amani

Watum amesema makubaliano ambayo bado hayajasitisha mapigano mashariki - yameweka ramani ya mazungumzo na makampuni ya Marekani kuhusu uwezekano wa miradi.

"Wengine wanaweza kuwekeza na wengine wasiwekeze. Na wakiwekeza, watafuata kanuni za uchimbaji madini," alisema.

DRC imewasilisha orodha ya miradi ya kimkakati kwa Marekani ambayo itapitiwa na kamati shirikishi katika wiki zijazo, amesema Makamu Waziri Mkuu Daniel Mukoko Samba alipokuwa Davos mwezi Januari.

Alipoulizwa kuhusu uhasama kati ya Marekani na China katika sekta ya madini ya Congo, Watum alisema DRC imejikita katika kuangalia vipaombele vya ndani, kama elimu na ajira kwa wananchi wake wapatao milioni 120.

"Hayo hayatuhusu. Tunafanya mambo yetu kama DRCC," amesema.

Rasilimali ambazo hazijatumika

Utajiri wa rasilimali za DRC bado haujatumika, huku asilimia 10 pekee ambayo ndio imeendelezwa, amesema Watum.

"Kuna nafasi ya kila mmoja," ameongeza, ikilinganishwa na nafasi ya sasa ya nchi katika soko la dunia ni kama Saudi Arabia katika soko la mafuta miaka ya 80.

Nchi hiyo ya Afrika Kati ina baadhi ya madini tajiri kabisa ya shaba, cobalt, coltan na lithiamu duniani na ilichangia asilimia 76 ya uzalishaji wa cobalt duniani mwaka 2024, kwa mujibu wa US Geological Survey.

Mahitaji ya madini haya yanaongezeka katika sekta za ulinzi, vituo vya takwimu vya akili bandia na mchakato wa mabadiliko ya nishati.