Rwanda: Zaidi ya wakimbizi 40 wa Burundi warejea makwao

Zoezi hilo linakuwa ni la 68 tangu mwaka 2020, ambapo zaidi ya wakimbizi 31,000 wa Burundi wamerudishwa nchini mwao.

By
Kundi hilo lilihusisha wakimbizi 62 waliokuwa wamehifadhiwa katika kambi ya Mahama iliyoko wilaya ya Kirehe na wengine 12 kutoka Kigali./Picha:Wengine

Kundi hilo lilihusisha wakimbizi 62 waliokuwa wamehifadhiwa katika kambi ya Mahama iliyoko wilaya ya Kirehe na wengine 12 kutoka jiji la Kigali.

Wakimbizi hao walirejea Burundi kupitia mpaka wa Nemba ulioko wilaya ya Busegera, kupitia mkakati maalumu wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi, chini ya uratibu wa serikali ya Rwanda na wadau wengine.

Zoezi hilo linakuwa ni la 68 tangu mwaka 2020, ambapo zaidi ya wakimbizi 31,000 wa Burundi wamerudishwa nchini mwao.

Kulingana na Gonzague Karagire, ambaye  ni afisa mradi wa katika wizara inayoshughulikia dharura nchini Rwanda, zoezi hilo ni la hiyari kwa wakimbizi ambao tayari walijiandikisha kwa mchakato huo.

"Mara baada ya kujisajili, tutaratibu na mataifa yao ili tukubaliane siku ya kuwapokea na sisi tutawezesha kurejea kwao," alisema.

Karagire aliongeza kuwa Rwanda inafanya kazi kwa ukaribu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kuhakikisha kuwa wakimbizi hao wanarejea kwa salama.