Erdogan na Macron wazungumzia vita vya Ukraine, migogoro ya kikanda na uhusiano wa mataifa mawili
Viongozi hao wa Uturuki na Ufaransa walijadili kuimarisha ushirikiano pamoja na yanayojiri Gaza, eneo la Caucasus na Syria, huku Erdogan akitoa wito kwa diplomasia mpya kufufua juhudi za amani zilizokwama kati ya Moscow na Kiev.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamezungumza kwa njia ya simu siku ya Jumatano kuangazia vita vya Urusi na Ukraine, migogoro ya kikanda na mustakabali wa uhusiano wa nchi hizo mbili, kulingana na Ofisi ya Rais wa Uturuki.
Mazungumzo hayo ya simu, yalioanzishwa kupitia maombi ya Macron, yaliangazia wigo mpana wa maendeleo ya kimataifa pamoja na ushirikiano kati ya Ankara na Paris, Ofisi ya Rais ilisema katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.
Erdogan alisisitiza kuwa kuimarisha ushirikiano kati ya Uturuki na Ufaransa "ni muhimu," akiongeza kwamba pande zote mbili zinapaswa kuendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuendeleza uhusiano.
Kumaliza vita nchini Ukraine
Kuhusu mzozo wa Urusu na Ukraine, Erdogan alisema Uturuki "inafanya kazi kwa juhudi kubwa" kuunga mkono amani ya haki na ya kudumu na kwamba Ankara inaendelea na mazungumzo yake na pande zote mbili ili kufufua mchakato wa Istanbul.
Kuhusu Uturuki, Erdogana aliendelea kusema, bado iko tayari "kutoa kila mchango unaowezekana" kufungua njia kuelekea mazungumzo.
Alisisitiza kwamba njia za kidiplomasia lazima zitumike ipasavyo ili kufikia amani ya kudumu na kwamba kuepuka vitendo vinavyoweza kuharibu mazingira ya kimataifa kutasaidia juhudi zinazoendelea za kusitisha mapigano.
Viongozi hao wawili pia wamezungumzia kuhusu yanayojiri katika eneo la Caucasus, Gaza na Syria.