Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu Tanzania
Daktari Mwigulu Nchemba anachukua nafasi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Wabunge watajadili na kupiga kura kuhusu uteuzi wa Dkt. Mwigulu Nchemba. / / Wengine
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Tanzania.
Taarifa za uteuzi huo zilitolewa Alhamisi na Spika wa Bunge, Mussa Zungu. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nchemba alikuwa Waziri wa Fedha, nafasi aliyokuwa nayo tangu mwaka 2021.
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, uteuzi wa Waziri Mkuu lazima uthibitishwe na Bunge kabla ya kuanza rasmi majukumu yake mapya.
Inatarajiwa kuwa wabunge watajadili na kupiga kura kuhusu uteuzi huo katika siku chache zijazo.