| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Ghana yawaondoa raia wake waliojeruhiwa katika shambulio la kigaidi Burkina Faso
Jeshi limesema katika kuwaondoa walikuwemo wafanyabiashara watatu wa nyanya waliojeruhiwa wakati wa shambulio hilo siku ya Jumamosi katika mji wa kaskazini mwa Burkina Faso wa Titao.
Ghana yawaondoa raia wake waliojeruhiwa katika shambulio la kigaidi Burkina Faso
Jeshi la Ghana linasema shughuli ya kuwaondoa watu ilitekelezwa Jumanne na Jeshi la Anga la Ghana. / Wengine
tokea masaa 3

Ghana imewaondoa raia wake waliojeruhiwa katika shambulio la kigaidi nchini Burkina Faso. Shambulio hili liliwaua wafanyabiashara saba wa Ghana, na tayari wamewafikisha manusura mjini Accra kwa matibabu, kulingana na taarifa iliotolewa na Jeshi la Ghana siku ya Jumamosi.

Jeshi linasema walioondolewa walikuwepo wafanyabiashara watatu wa nyanya raia wa Ghana ambao walijeruhiwa wakati wa shambulio la Jumamosi katika mji wa kaskazini mwa Burkina Faso wa Titao.

“Shughuli hiyo ilitekelezwa Jumanne na Jeshi la Anga la Ghana,” taarifa hiyo ilisema. “Waliojeruhiwa wamepelekwa katika Hospitali ya Jeshi ambapo watafayiwa vipimo na kutibiwa.”

Jeshi limetuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wale waliouawa na kuwatakia afuweni ya hataka wale waliojeruhiwa.

Maafisa wa serikali wanasema waliouawa walikuwa sehemu ya kundi la wafanyabishara wa nyanya raia wa Ghana waliokuwa wamesafiri Burkina Faso kwa shughuli za kibiashara wakati waliposhambuliwa na wapiganaji katika mji huo.

Biashara isio rasmi

Kwa kawaida wafanya biashara huvuka mpaka kununua nyanya na bidhaa zingine za kilimo kama utaratibu wa muda mrefu wa biashara isio rasmi kati ya nchi hizo mbili.

Burkina Faso imekaabiliwa na vurugu nyingi katika miaka ya hivi karibuni kutoka kwa makundi ya kigaidi yenye uhusiano na makundi ya Al Qaeda na Daesh, huku mashambulio yakienea kote eneo la Sahel na kuwalenga raia pamoja na shughuli zao za kiuchumi.

Maafisa wa Ghana wanasema bado wanajadiliana na mamlaka za Burkina Faso huku juhudi za kuwatibu manusura na kusaidia familia za wale waliopoteza wapendwa wao.

CHANZO:AA