Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Gabon, Jean-Claude Mendome, mitandao hiyo ilikuwa ikihusika kwa kiasi kikubwa na usambaaji wa taarifa potofu, mmonyoko wa maadili na kutishia usalama wa taifa hilo.
Msemaji huyo aliongeza kuwa “maudhui yasiyofaa, ya kashfa, chuki na matusi” yanadhoofisha heshima ya binadamu, maadili ya umma, mshikamano wa kijamii, uthabiti wa taasisi za Jamhuri na usalama wa taifa.
Hata hivyo mdhibiti huyo alisema "uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na uhuru wa maoni na ukosoaji," imesalia kuwa "haki ya kimsingi iliyowekwa nchini Gabon".
Chini ya mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa, Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema amekabiliwa na wimbi la kwanza la machafuko ya kijamii, huku walimu na watumishi wengine wa umma wakitishia kugoma.
















