Wanajeshi 33 wauawa katika shambulio la kigaidi nchini Burkina Faso

Taarifa kutoka kwa jeshi inasema kuwa kikosi kilichoweka kambi yake katika jimbo la Gourma kilishambuliwa na watu wasiojulikana.

By Yusuf Dayo
Wanajeshi wauwawa katika shambulio Archives Reuters / Others

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa magaidi takriban 40 walidhibitiwa katika makabiliano hayo lakini wanajeshi 33 waliuawa huku wengine 12 wakijeruhiwa.

Burkina Faso, mojawapo ya mataifa maskini zaidi barani Afrika, limekuwa likilengwa na magaidi wanaohusishwa na wanamgambo wa Al Qaeda na DAESH walioweka kambi zao katika nchi jirani ya Mali tangu mwaka wa 2015.