7 Wafariki baada ya mgodi kuporomoka nchini Ghana

Maafisa wa Ghana bado hawajazungumzia ajali hiyo, lakini kumekuwa na msako mkali dhidi ya migodi haramu nchini humo

By Yusuf Dayo
Mvua kubwa iliyonyesha nchini Ghana inashukiwa kusababisha kuporomoka kwa mgodi / Picha: Reuters / Reuters

Watu saba wamefariki huku wengine 17 wakinasa katika mgodi ulioporomoka katika wilaya ya kaskazini ya Birim, nchini Ghana, vyombo vya habari vimeripoti.

Waokoaji wamefanikiwa kuwatoa watu wawili wakiwa hai kutoka mgodi huo.

Kwa mujibu wa waandishi wa habari katika eneo hilo, vyombo vya habari vimezuiwa na wachimba migodi wanaoendesha shughuli hio ya uokoaji kufika katika mgodi au kuchukua picha zozote za ajali hiyo.

Bado sababu halisi haijajulikani ya kuporomoka kwa mgodi huo japo inaaminiwa kuwa mvua kubwa inayoendelea kunyesha huenda ndio sababu.