Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi afariki akiwa na miaka 86
Alipatwa na matatizo yanayo husiana na leukemia yaani saratani ya damu ya muda mrefu ambapo hapo awali haikufahamika
Berlusconi alikuwa amelazwa katika hospitali ya Milan ya San Raffaele wiki iliyopita kutokana na matatizo yanayohusishwa na saratani ya damu / Picha: AFP / AFP
Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi amefariki Jumatatu akiwa na umri wa miaka 86.
Berlusconi alikuwa amelazwa katika hospitali ya Milan ya San Raffaele wiki iliyopita kutokana na matatizo yanayohusishwa na saratani ya damu ya muda mrefu ambayo haikujulikana hapo awali, shirika la habari la Italia ANSA liliripoti.