| Swahili
AFRIKA
3 DK KUSOMA
Sierra Leone: Bio anahimiza utulivu, Kamara awashukuru wapiga kura
Raia wa Sierra Leone wanasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi baada ya kupiga kura Jumamosi, Juni 24.
Sierra Leone: Bio anahimiza utulivu, Kamara awashukuru wapiga kura
Wagombea 13 walikuwa kwenye karatasi ya kura katika uchaguzi wa rais wa 2023 Sierra Leone. / Picha: Reuters / Reuters

Rais Julius Maada Bio amewataka raia wa Sierra Leone kuwa watulivu wakati shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea kufuatia uchaguzi wa Jumamosi.

"Tunaposubiri kutangazwa rasmi kwa matokeo kutoka kwa Tume ya Uchaguzi ya Sierra Leone, ninahimiza kila mtu kuwa mtulivu, kuweka imani katika mifumo na kuendelea kulinda amani na umoja wetu," alisema kwenye Twitter siku ya Jumapili.

Samura Kamara, mmoja wa wagombea 13 katika uchaguzi wa rais, amewataka raia wa Sierra Leone "kuungana na kusonga mbele."

"Shukrani za dhati kwa taifa na kila mpiga kura ambaye alitoa sauti yake [kusikika] katika chaguzi zetu za urais, ubunge na mitaa. Kushiriki kwako ndiko kunakochochea demokrasia yetu,” Kamara alisema kwenye Twitter.

Ushindani wa karibu

Kura za maoni zinatabiri mchuano wa karibu kati ya Rais Bio na Kamara, mgombea wa upinzani.

Takriban watu milioni 3.4 walikuwa wamejiandikisha kuwa wapiga kura kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Juni 24, 2023 wa Sierra Leone.

Upigaji kura kwa kiasi kikubwa ulikuwa wa amani, huku mifuko ya ghasia na madai ya wizi yakiripotiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Katika taarifa yake siku ya Jumamosi, tume ya uchaguzi ilisema ghasia zilifanywa dhidi ya wafanyakazi wake wakati wa usafirishaji wa nyenzo za uchaguzi, na kuyataja mashambulio hayo kuwa "bahati mbaya".

"Hii ni hali ya kusikitisha kwa sababu uhamishaji wa nyenzo hizi unafanywa kwa mujibu wa sheria," tume hiyo ilisema.

Zoezi la 'Uwazi'

Kuhusu madai ya ujazo wa kura na aina nyingine za wizi, tume ya uchaguzi ilisema madai hayo si ya kweli kwa sababu "maafisa wa polisi na waangalizi wa uchaguzi walikuwepo katika vituo vyote vya kupigia kura."

Kucheleweshwa kwa kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura kulishuhudiwa katika maeneo ya magharibi mwa nchi na wilaya za mijini, na kusababisha rabsha miongoni mwa wapiga kura. Tume ya uchaguzi ilisema ilipokea nyenzo za kupigia kura kuchelewa, na kusababisha kucheleweshwa.

Baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura saa kumi na moja jioni siku ya Jumamosi, kuhesabu kura kulianza.

Uhesabuji kura, hata hivyo, ulianza saa nane usiku siku ya Jumapili katika vituo vingi nchini, huku zoezi hilo likitarajiwa kuchukua zaidi ya siku moja kukamilika.

Bio, ambaye amekuwa Rais wa Sierra Leone tangu Aprili 2018, anatarajia kumpiku mpinzani wake mkuu Kamara kwenye mechi ya marudiano.

Bio kutoka Chama cha Sierra Leone People's Party (SLPP) alipata kura milioni 1.3 na kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2018, huku Kamara wa Chama cha All People's Congress (APC) akiibuka wa pili kwa kura milioni 1.2.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya watoa tahadhari kuhusu maandamano ya Juni 25
Mshambuliaji wa Côte d'Ivoire Wahi hatimaye apata viza ya Canada baada ya kunyimwa awali
Wabunge wa Zimbabwe waunga mkono sheria ya kuongeza muda wa rais madarakani
Madaktari Tanzania waja na mikakati dira 2050 kuimarisha  huduma za afya
Tanzania kinara wa simba, nyati barani Afrika
Milio ya risasi yaripotiwa karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Niger
IGAD yataka mamlaka ya Somalia kuheshimiwa huku ushirikiano kati ya Israel na Somaliland ukiendelea
Kenya, Marekani zinakaribia kufikia makubaliano muhimu ya madini, asema Rais Ruto
Kwa nini ushirikiano wa Somalia-Uturuki ni kielelezo cha sera ya kigeni ya karne ya 21
Ugavi wa damu salama unaimarika duniani kote huku uchangiaji wa damu kwa hiari ukiongezeka kwa 85%
Mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda anakanusha mashtaka katika kesi ya ICC
Watu 9 wamefariki baada ya basi la abiria kuigonga treni ya mizigo nchini Zimbabwe
Mlipuko wa Ebola huenda ukawa mbaya zaidi kuwahi kutokea, Afrika CDC yaonya
Bunge lamtengenezea njia Rais wa DRC Tshisekedi kugombea muhula wa tatu
Wanaume wenye silaha wamuondoa mwanamke, mtoto kutoka kliniki ya Ebola DRC, mamlaka inasema
Marekani imempa uhamiaji wa kudumu aliyekuwa waziri wa fedha wa Ghana, wakili wake anasema
Nigeria imewakamata watu wanane kwa kueneza habari potofu
Viongozi wa G7 watoa wito wa 'uratibu wa pamoja' kukabiliana na mlipuko wa Ebola nchini DRC, Uganda
Shirika la Fedha Afrika kumpa Dangote milioni $600 kwa ajili ya miradi ya mbolea Nigeria, Ethiopia
Siasa za lawama: Kwa nini wahamiaji wamekuwa walengwa katika mzozo wa kiuchumi wa Afrika Kusini