| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
“NATO inapaswa ‘kubadilika’ ili kukabiliana na changamoto za vita vya kisasa: Burhanettin Duran
Mkuu wa Mawasilano wa Uturuki Burhanettin Duran amesema NATO inahitaji kuzingatia nguvu ya kuzuia vitisho na usimamizi thabiti wa migogoro, wakati huo huo Uturuki inaendelea kukuza amani katika maeneo mbalimbali.
“NATO inapaswa ‘kubadilika’ ili kukabiliana na changamoto za vita vya kisasa: Burhanettin Duran
Mkutano wa "Nafasi ya Uturuki katika NATO", uliosimamiwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki na SETA, umefanyika Aprili 9 2026. / / AA
tokea masaa 5

Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki amesema kuwa NATO inapaswa kuendana na uhalisia wa vita vya kisasa vya kimuundo kwa kutumia mbinu thabiti, ya kina, na kuzingatia usimamizi madhubuti wa migogoro.

Akibainisha tofauti za mikakati ya ulinzi kati ya nchi wanachama, Burhanettin Duran alibainisha kuwa tofauti hizi mara nyingi husababisha kutokuelewana ndani ya Umoja wa NATO.

“NATO inapaswa kujiboresha kwa ajili ya vita vya kisasa vya kimuundo, kwa kuzingatia uthabiti, nguvu ya kuzuia vitisho, na usimamizi thabiti wa migogoro,” alisema siku ya Alhamisi.

Akizungumza katika mkutano wa "Nafasi ya Uturuki katika NATO: Kujipanga Kimkakati kwa Muungano Imara" jijini Ankara, alisema Uturuki ina uwezo wa kutoa mchango mkubwa kwa Umoja huo.

“Uturuki, katika muktadha huu, ina nguvu na uwezo wa kutoa michango mikubwa kwa NATO, kama ilivyokuwa awali na inapanga kuendelea kufanya hivyo katika siku za usoni,” aliongeza.

Uturuki ndani ya NATO

Akibainisha jinsi Umoja huo ulivyobadilika kwa miongo kadhaa, Burhanettin Duran alisisitiza kuwa NATO ilianzishwa awali kwa lengo la kukabiliana na tishio la Umoja wa Kisovieti na ilitimiza jukumu lake kikamilifu baada ya Mwisho wa Vita Baridi.

Alionya kuwa dunia ya leo inakabiliwa na mgawanyiko tata na changamoto nyingi katika mpangilio wa kimataifa.

“NATO, tena, sasa inazidiwa na shinikizo la kubadilisha mtazamo wake,” alisema Duran.

Akionyesha migogoro ya kisasa, aliashiria mizozo nchini Ukraine, vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, na mvutano wa Mashariki ya Kati.

Duran pia alisisitiza nafashi ya kimkakati ya Uturuki na mtazamo wake wa usalama wa pande zote.

“Uturuki, katika mchakato huu, imefanya kazi siyo tu kulinda mipaka yake bali pia kuimarisha amani na usalama katika kanda na duniani kote,” alisema.

Alibainisha juhudi za kidiplomasia za Uturuki chini ya uongozi wa Rais Recep Tayyip Erdogan, akisema Uturuki ilichukua hatua chanya katika mgogoro kati ya Urusi na Ukraine na katika kufanikisha suluhisho la haki katika mgogoro wa Karabakh.

Kando na eneo lake, Uturuki imekuwa ikikuza amani barani Afrika, ikiwahimiza wapiganaji wakiwemo pande mbili zinazozana kuleta utulivu katika bara hilo

CHANZO:TRT World and Agencies