Urusi imeituhumu Ukraine kwa kushambulia mitambo yake kusafishia mafuta iliyo katika eneo la Ryazan, kilichopo kilomita 180, kusini mwa Moscow.
Shambulizi hilo, linakuja baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kuliambia gazeti la Uingereza la Financial Times, kuwa nchi yake inalenga kushambulia mitambo na viwanda vya Urusi.
Wakati huo huo, Urusi imeendelea kuvishambulia vituo vya nishati vya Ukraine, na kusababisha katizo kubwa la umeme nchini humo.
ZILIZOPENDEKEZWA
Katika mahojiano yake na Financial Times, Zelensky alisema kuwa, imechoshwa na mashambulizi yanayofanywa na Urusi, ikisisitiza kuwa italipa kisasi.
Hakuna majeruhi wowote walioripotiwa wkaati wa tukio hilo, kulingana na Gavana wa Ryazan, Pavel Malkov.
CHANZO:AFP

















