"Mkataba wa Ushirikiano wa Sekta ya Ulinzi" ulitiwa saini kati ya Kenya na Uturuki

Mkataba ulitiwa saini kati ya Uturuki na Kenya ili kuweka uhusiano wa kitaasisi katika sekta ya ulinzi na kusambaza, kuendeleza na kuzalisha kila aina ya bidhaa na huduma za sekta ya ulinzi zinazohitajika na vikosi vya usalama.

By trtafrikaswa
Makubaliano hayo yalisainiwa kati ya Rais wa Taasisi ya Ulinzi ya Raisi, Haluk Görgün, na Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Aden Duale. Picha: AA / Others

Sherehe ya kusaini makubaliano kati ya nchi mbili ilifanyika katika Maonyesho ya 16 ya Kimataifa ya Viwanda vya Ulinzi (IDEF).

Makubaliano hayo yalisainiwa kati ya Rais wa Taasisi ya Ulinzi ya Raisi, Haluk Görgün, na Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Aden Duale.

Görgün alisema kuwa IDEF inacheza jukumu muhimu katika kukidhi mahitaji ya nchi za kirafiki na kikanda katika tasnia ya ulinzi na kuendeleza ushirikiano na nchi nyingine.

Akieleza kuwa ushirikiano kati ya Uturuki na Kenya utaanzishwa rasmi kupitia makubaliano hayo, Görgün alisema:

"Makubaliano hayo yanajumuisha kanuni za shughuli za ushirikiano wa pande zote kati ya nchi hizo mbili katika tasnia ya ulinzi.

Makubaliano yetu yanajumuisha usambazaji moja kwa moja, maendeleo, uzalishaji, na utoaji wa aina zote za bidhaa na huduma za tasnia ya ulinzi zinazohitajika na taasisi za usalama za pande zote. Pia, mauzo, ukarabati, uboreshaji wa mifumo na jukwaa zilizopo, uhamishaji wa teknolojia, mafunzo, na kubadilishana taarifa na nyaraka."