Picha za marais 13 wa Afrika, Waziri Mkuu mmoja ambao wamevaa sare za jeshi karibuni

Viongozi wa Afrika wasiopungua 14 wamekuwa wakivaa sare za jeshi hadharani katika miaka ya hivi karibuni, magwanda ambayo hufanya watu kuwaangalia kwa makini.

By Brian Okoth
Marais wa Ghana, Tanzania, na Kenya ni miongoni mwa viongozi karibu 14 Afrika ambao wameva sare za jeshi hadharani. / Wengine

Viongozi wa Afrika wasiopungua 14 wamekuwa wakivaa sare za jeshi hadharani katika miaka ya hivi karibuni, magwanda ambayo hufanya watu kuwaangalia kwa makini.

Viongozi wa kiraia ambao wamekuwa wakivaa sare za jeshi katika siku za hivi karibuni ikiwemo Marais William Ruto wa Kenya, Duma Gideon Boko (Botswana), Samia Suluhu Hassan (Tanzania), Paul Kagame (Rwanda), Netumbo Nandi-Ndaitwah (Namibia), John Mahama (Ghana), and Bassirou Diomaye Faye (Senegal).

Wengine ni Hassan Sheikh Mohamud (Somalia), Umaro Sissoco Embalo (Guinea-Bissau), Cyril Ramaphosa (South Africa), Yoweri Museveni (Uganda), Salva Kiir (South Sudan), Adama Barrow (The Gambia), and Ethiopia's Prime Minister Abiy Ahmed.

Katika nchi kadhaa za Afrika, mkuu wa nchi anapewa cheo cha heshima cha jenerali wa nyota tano, kuonesha ishara ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

Mamlaka ya moja kwa moja

Pamoja na kuwa cheo hicho kinaonesha umuhimu wa mhusika katika operesheni za kijeshi, marais wa kiraia hawana mamlaka kamili ya kuamrisha taifa liingie katika vita.

Kwa mfano, Marekani, rais — ambaye ni amiri jeshi mkuu — anaweza kutoa amri moja kwa moja kwa baadhi ya operesheni za kijeshi, kama kupeleka majeshi, lakini hawawezi kuamrisha nchi kwenda vitani moja kwa moja.

Uwezo huu ni wa Bunge la Congress, ambalo linaidhinisha watu kwenda vitani na pia wanasimamia bajeti ya jeshi.

Nchini Uingereza, tawala la ukoloni la nchi karibu 17 za Afrika, mfalme, ambaye ni mkuu wa nchi, ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya nchi.

Idhini ya bunge

Tofauti na Marekani, ambapo rais wa nchi hawezi kuamua peke yake nchi iende vitani, Uingereza mfalme, ambaye anatambulika kuwa "huru," ndiye "pekee anaweza kutangaza wakati wa vita na amani," mtandao wa Familia ya Kifalme unasema.

Hata hivyo, mfalme anatekeleza hilo kufuatia ushauri wa mawaziri wakati wa kutangaza vita.

Nchi nyingi barani Afrika zinaiga utaratibu wa Marekani, ambapo bunge linaidhinisha au kukataa nchi kwenda vitani.

Kutembelea maeneo ya vita

Kuwapandisha vyeo na kuwateua wanajeshi, mkuu wa nchi kufuatia ushauri baraza la ulinzi la nchi.

Pamoja na majukumu makubwa ya kiutawala, wakati mwingine amiri jeshi mkuu wa majeshi yote hutembelea vikosi vyake katika maeneo ya vita.

Kwa mfano, mwezi Septemba 2023, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitembelea mji wa kati wa Mahas, ambapo jeshi lilikuwa linapigana na kundi la kigaidi la Al Shabab. Rais Mohamud alikuwa amevaa sare ya kijani ya jeshi.

Mwaka mmoja baadaye, kiongozi huyo wa Somalia pia alionekana amevaa sare ya jeshi akiwa katika makao makuu ya jeshi katika mji mkuu, Mogadishu, alipokuwa na kikao cha dharura cha usalama kuhusu mapambano dhidi ya Al Shabab.

'Ujumbe mzito kwa utayari wa taifa'

Mwandishi wa habari nguli wa Misri Khaled Mahmoud aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X Septemba 1, 2024: "Kuamua kwa rais wa (Somalia) kuvaa sare za jeshi kunatuma ujumbe mzito wa kuwa tayari na mapambano, akisisitiza utayari ambao anauhimiza sasa hivi."

Mwezi Mei 16, 2017, Rais Kiir alivaa sare za kijeshi wakati wa siku ya kuadhimisha majeshi nchini humo, inayoadhimishwa kila mwaka kuwakumbuka wanajeshi waliouawa eneo la Bor, jimbo la mashariki la Jonglei, Sudan Kusini, in 1983.

Tukio hilo lilichochea vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili vilivyosababisha Sudan Kusini kupata uhuru wake Julai 2011.

'Pamoja na vikosi'

Pamoja na kuwa hakuna sheria inayowazuia marais wa kiraia wa Afrika kuvaa sare za jeshi hadharani, katika nchi za nje kama vile Lithuania, rais wa kiraia nchini humo alilazimika kutetea uamuzi wake wa kujitokeza hadharani akiwa na sare za jeshi.

17 Septemba, 2019, Rais wa Lithuania Gitanas Nauseda, akiwa amevaa nguo za kijeshi alikutana na wanajeshi katika mji wa katikati ya nchi wa Rukla, aliwaambia waandishi wa habari: "Nataka niungane na vikosi vyetu kwa moyo wangu wote, na kama ningekuja hapa nimevaa viatu vya kupendeza na suti ili nipate taarifa, isingekuwa picha nzuri”

Katika mataifa ya Magharibi, maamuzi ya viongozi wa nchi kuvaa sare za kijeshi hadharani huibua majadiliano, huku wakosoaji wakiteta kuwa raia hawaruhusiwi kuvaa sare za kijeshi, kwa misingi ya utaratibu wa kidemokrasia ambayo yanasisitiza kuyapa majukumu ya utawala bora ya taifa kwa taasisi zisizo za kijeshi.

Hata hivyo, barani Afrika, viongozi wa taifa na serikali mara moja moja huvaa sare za kijeshi kwa lengo la kuonesha kuwaunga mkono wanajeshi, jambo ambalo limekuja kukubalika.

Hapa kuna picha za viongozi wa Afrika wakiwa wamevaa sare za jeshi hadharani:


SOURCE: TRT Afrika