| Swahili
AFRIKA
12 DK KUSOMA
Siku ya Kibinadamu Duniani: Kisa cha kushangaza cha ukoloni wa Ufaransa barani Afrika
Katika Siku ya Kibinadamu Duniani, hebu tuangalie kwa undani jinsi ukoloni wa Ufaransa ulivyoiba mustakabali wa mataifa mengi ya Kiafrika na iwapo misaada inayopigiwa debe na nchi za Magharibi inawasaidia au kuwaumiza.
Siku ya Kibinadamu Duniani: Kisa cha kushangaza cha ukoloni wa Ufaransa barani Afrika
Urithi wa ukoloni wa Ufaransa bado unaunda hali halisi ya kisiasa, kiuchumi, na kitamaduni ya nchi nyingi za Kiafrika. / Picha: Jalada la AA / Others

NA ZEYNEP CONKAR

Huku Siku ya Kibinadamu Duniani ikiadhimishwa duniani kote tarehe 19 Agosti, mitandao ya kijamii itakuwa na maoni mengi kuhusu nchi na maeneo yaliyoathiriwa na migogoro, ukame na majanga ya asili. Na sehemu kubwa ya umakini ingetolewa kwa Afrika.

Ingawa misaada ya kibinadamu inahitajika katika sehemu nyingi za dunia, ni bara la Afrika ambalo daima linahitaji uangalizi wa ziada, hasa kwa sababu ndilo bara maskini zaidi duniani lenye Pato la Taifa la $ 1591 kwa kila mtu kinyume na $ 63,543 iliyorekodiwa nchini Marekani pekee.

Afrika haikutarajiwa kuwa masikini. Ilifanywa maskini kwa makusudi. Bara lenye rasilimali nyingi na utajiri mkubwa wa asili, mahali hapo palikuwa windo la madola ya kifalme ya Ulaya, na Ufaransa ikifanya uhalifu mbaya zaidi wa kikoloni.

Kuanzia Algeria, ukoloni ulieneza misimamo yake katika eneo lote na baadaye, mamlaka za Ulaya ziliweka msingi wa kazi za moja kwa moja kupitia Mkutano wa Berlin wa 1884, ukigawanya bara

"Mipaka yote ilichorwa kwenye meza za Ulaya - huko Paris, London, Madrid, Lisbon, Berlin, Roma na Brussels," anasema Profesa Ahmet Kavas, Balozi wa zamani wa Uturuki nchini Senegal na Chad na mkuu wa zamani wa Kitivo cha mafunzo ya sayansi ya siasa, Chuo Kikuu cha Istanbul Medeniyet.

Kuelewa historia ya Afrika si kamili bila kuzama katika uwepo wa kihistoria wa Ufaransa na ushawishi wa kudumu katika eneo hilo.

Kudhibiti Afrika kupitia Waafrika

Wakati uwepo wa Wafaransa barani Afrika ulianza karne ya 17, kipindi kikuu cha upanuzi wa kikoloni kilianza na kukaliwa kwa Algeria mnamo 1830. Vitendo vya unyonyaji vilianza kutekelezwa nchini humo, pamoja na kazi ya kulazimishwa, ili kuweka nishati ya watu wote wa Algeria. katika huduma ya utawala wa Ufaransa.

Sera kama hizo za kibabe zilitekelezwa na Uingereza katika sehemu fulani za Afrika mabazo ilikaliwa kwa mabavu na mamlaka ya kifalme.

"Mamilioni ya Waafrika walihamishwa na Waingereza na Wafaransa katika nyanja mbalimbali za Vita vya Kwanza vya Dunia na Vita vya Kidunia vya pili, na pia kutumika kama kazi ya kulazimishwa kwa ajili ya ujenzi wa miji ya Ulaya iliyoharibiwa baada ya vita," Kavas anasema.

Baada ya Mapinduzi ya Viwanda, kulikuwa na mahitaji makubwa ya malighafi na masoko mapya barani Ulaya. Ufaransa iliona Afrika kama soko la kutumia malighafi na pia chanzo cha nguvu kazi, kulingana na Dk Ensar Kucukaltan, Mratibu Mkuu wa Kituo cha Uratibu na Mafunzo cha Afrika (AKEM).

"Ufaransa ililenga kuhakikisha uhamishaji wa rasilimali za chini na juu ya ardhi kutoka Afrika hadi katika maeneo iliyomiliki na ilifanikisha hili sio kwa kuongeza vikosi vya kijeshi lakini kwa kusajili viongozi wa eneo hilo kufanya kazi kwa maslahi ya Ufaransa," Kucukaltan anasema, akiongeza kuwa "waliweza kudhibiti Waafrika kwa watu wa Kiafrika”.

Kuanzia kuhalalisha mauaji na mateso hadi kupora rasilimali zake, Ufaransa ililitendea bara hilo ukatili kiasi kwamba vizazi vyake vijavyo havikuweza kujirejesha katika hadhi yake duniani.

Urithi wa ukoloni wa Ufaransa bado unaunda hali halisi ya kisiasa, kiuchumi, na kitamaduni ya nchi nyingi za Kiafrika.

Enzi ya ukoloni mamboleo

Baada ya mataifa kadhaa ya Kiafrika kutangaza uhuru wao katika miaka ya 1960, Ufaransa ilitafuta njia za kuendelea kutumia rasilimali zao. Waliweka Kifaransa kuwa lugha rasmi na lugha ya kufundishia shuleni, jambo ambalo liliwasaidia katika kuwakuza wasomi wenyeji waliofunzwa maadili ya Magharibi.

Kisha maafisa wa Ufaransa walifanya makubaliano na mashirika yenye nguvu ya kibepari na kuanza kukusanya faida kupitia unyonyaji unaoendelea wa rasilimali za Kiafrika - mafuta, gesi asilia, urani, dhahabu, almasi, mazao ya kilimo na madini mengine.

"Katika suala la athari za kudumu, ninaamini Ufaransa ilichukua hatua muhimu zaidi katika zama za baada ya ukoloni, hasa katika suala la lugha na elimu. Hata wale wanaoipinga Ufaransa wanapaswa kueleza upinzani wao kwa Kifaransa," anasema Kavas.

Afrika iliingia katika enzi ya ukoloni mamboleo licha ya mataifa mengi ya baada ya ukoloni kupata uhuru wa kujitawala kutoka kwa nguvu za kikoloni. Muktadha huu wa ukoloni mamboleo ni msingi wa kuelewa changamoto nyingi zinazokabili Afrika leo.

"Wakati mataifa ya kikoloni yalipoanza kujiondoa kutoka Afrika, ilikuwa dhahiri kwamba walianzisha mashirika na miundo fulani ili kuendeleza mfumo huo kabla ya kuondoka," Kucukaltan anasema.

"Hali ya Niger na mapinduzi ya hivi karibuni iko katika hali hii. Ufaransa inapata zaidi ya asilimia 90 ya uranium inayozalishwa kutoka Niger. Kwa hiyo, licha ya kukaa kwenye rasilimali nyingi za urani, theluthi mbili ya watu wanapata chini ya dola mbili kwa siku, na kuishi katika mazingira magumu."

Hali kama hiyo, anasema Kucukaltan, inaweza kuzingatiwa katika baadhi ya maeneo ya makoloni ya Afrika Magharibi na Kati yanayonyonywa na Ufaransa.

"Ufaransa inafungamanisha kuendelea kwa tawala za Kiafrika kwa maslahi yake binafsi, pia. Ikiwa una uhusiano mzuri na Ufaransa na kutii sheria zao, wanakuruhusu kubaki madarakani".

Kavas alidokeza kuwa Ufaransa inakataa kukubali kuwa sera zake barani Afrika ni sawa na ukoloni mamboleo.

"Nchi hiyo badala yake inadai kuwa 'ushirikiano' na kuutaja kama uhusiano wa serikali na nchi," Kavas anasema.

Ufaransa bado inadumisha uwepo wa kijeshi katika eneo la Sahel na Afrika ya Kati pamoja na Chad, Mali na Niger. Zaidi ya hayo, Ufaransa inaendelea kutoa ushawishi juu ya michakato ya kisiasa katika kanda.

Msaada wa kibinadamu

Miongo kadhaa ya unyonyaji wa Ufaransa umeacha sehemu kubwa ya bara katika uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu.

Ingawa Ufaransa ni nchi wafadhili wa misaada ya maendeleo inayofungamana na Afrika, wakosoaji wengi wanasema inatumia michango hiyo kwa manufaa ya kisiasa.

"Chini ya utumwa, watu walipoteza sio ardhi yao tu bali pia utamaduni wao, mtindo wao wa maisha, na kujistahi. Wakati watu wanaambiwa kwamba hawana uwezo wa kufanya chochote wao wenyewe, inawaweka katika hali ya kuhitaji msaada,” Kucukaltan anaongeza.

Kucukaltan anasema kuwa misaada ya kibinadamu inayokwenda Afrika tangu mataifa yenye nguvu ya kikoloni yalijiondoa katika bara hilo inahitaji kuchunguzwa kwa kina.

Wakati katika nadharia, anasema, misaada ya maendeleo ambayo nchi za Magharibi hutuma barani Afrika inakusudiwa kukuza ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla, inachangiwa kwa kiasi kikubwa na matarajio ya ukoloni mamboleo.

“Kwa kweli, hili limechunguzwa kwa kina katika tafiti zilizofanywa, hasa kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo misaada ya maendeleo ilichunguzwa kwa umakini. Swali la kama ina manufaa kweli lilizushwa.

Ukizungumza na Waafrika wengi, watakuambia kwamba wameona madhara zaidi kuliko mema kutokana na misaada ya maendeleo ya Magharibi," Kucukaltan anasema.

Uchunguzi mwingi huru umebaini kuwa misaada ya Magharibi imesababisha ukandamizaji zaidi, mauaji ya wakosoaji na ubadhirifu mkubwa barani Afrika, na kusababisha kukosekana kwa utulivu badala ya kuinua walio masikini.

Afrika, kama ilivyo

Ingawa bado inakumbwa na jinamizi la enzi za ukoloni, Afrika ni zaidi ya hili.

Wazo la kutokuwa n aimani na Waafrika linaweza kueleweka kama kuwa Waafrika hawawezi kutimiza chochote peke yao, ambayo kwa bahati mbaya imekuwa sehemu ya ubaguzi wa rangi, haswa huko Marekani.

"Inajenga dhana kwamba Afŕika inahusishwa tu na ukame, njaa, na mizozo, na kwamba hakuna kitu chanya zaidi ya hayo, isipokuwa hitaji la msaada, misaada ya kibinadamu,” anasema Kucukaltan.

Hata hivyo, mataifa kadhaa ya Afrika yamepata maendeleo mazuri katika kukuza uchumi wa viwanda kwa kuzingatia viwanda vinavyoongozwa na mauzo ya nje. Sehemu ya uzalishaji barani Afrika ya pato la taifa imeongezeka kutoka asilimia 9.4 mwishoni mwa miaka ya 2000 hadi asilimia 11.1 mwaka 2018.

Kuanzia uzalishaji wa nguo hadi kusafirisha maua kote ulimwenguni, bara limeshawishi ulimwengu kuwa lina mengi ya kutoa na halitaonekana tena kutoka kwa darubini ya mizozo na umaskini.

Ili kujiondoa kutoka kwa nguvu za ukandamizaji wa Magharibi, bara Afrika limekaribia mataifa mengine yanayoibuka kama vile Uchina, Uturuki na India.

Ushirikiano wa Uturuki na Afrika

Uturuki ina jukumu kubwa barani Afrika, linalojumuisha nyanja zote za kidiplomasia, kiuchumi, kitamaduni na kibinadamu.

"Uturuki inashikilia moja ya viwango vya juu zaidi vya uhusiano wa kidiplomasia na balozi 44 barani Afrika. Kuna makampuni mengi ya Kituruki ambayo yanaendesha bandari, na viwanja vya ndege barani Afrika. Shirika la ndege la Uturuki linalosafiri kwa zaidi ya nchi 40 za Kiafrika ni urahisishaji muhimu kwa mawasiliano ya Afrika kimataifa," Kavas anasema.

"Uturuki huenda kwenye pembe za mbali zaidi, kufungua visima, kutoa msaada wa chakula, kuanzisha vituo vya afya, kusaidia elimu na mengi zaidi".

Kulingana na Ripoti ya Global Humanitarian Assistance 2022 iliyoandaliwa na shirika lenye makao yake makuu Uingereza Development Initiatives, uturuki inashika nafasi ya lwanza duniani katika usaidizi wa kibinadamu kulingana na pato lake la jumla la taifa, ikiwa na dola bilioni 5.587.

Uturuki ilishika nafasi ya tatu katika orodha hiyo mnamo 2013, 2014, na 2015, ya pili 2016 na 2020, na ya kwanza mnamo 2017, 2018, na 2019. Mnamo 2020, Uturuki pia ilipata nafasi yake kama nchi inayotoa kwa wingi zaidi misaada inayohusiana na pato lake la taifa.

Kucukaltan aliunga mkono maoni kama hayo, akisema Ankara daima imekuwa ikisukuma simulizi inayopendelea watu wa Afrika.

"Hasa wakati wa mgogoro wa Somalia katika miaka ya 2010, tunaweza kuona wazi umuhimu wa Uturuki. Wakati Rais wa Uturuki Erdogan aliposafiri kwenda Mogadishu, Somalia pamoja na baadhi ya mawaziri na manaibu, ilielekeza usikivu wa vyombo vya habari vya Magharibi kuelekea Somalia,” anasema.

Akikumbuka safari zake barani Afrika, Kucukaltan anasema watu kote barani Afrika wanaitazama Uturuki kwa mtazamo tofauti kinyume na mtazamo wao wa mataifa ya Magharibi.

"Nia na umakini unaoonyeshwa kwetu (Waturuki) ni tofauti kabisa. Na urafiki huu unapatikana kupitia kazi ya serikali ya Uturuki na mashirika yasiyo ya kiserikali "

CHANZO:TRT World