| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Mapipa milioni 400 ya mafuta kutoka akiba ya dharura kuokoa hali ya uhaba duniani
Wanachama wa IEA wana hifadhi ya dharura ya zaidi ya mapipa bilioni 1.2 na mapipa milioni 600 zaidi ya hisa ya viwanda yakiwa chini ya wajibu wa serikali.
Mapipa milioni 400 ya mafuta kutoka akiba ya dharura kuokoa hali ya uhaba duniani
Wanachama wa IEA wana hifadhi ya dharura ya zaidi ya mapipa bilioni 1.2 ya mafuta / AP
12 Machi 2026

Nchi 32 Wanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati, IEA, walikubaliana kwa kauli moja 11 Machi 2026 kutoa mapipa milioni 400 ya mafuta katika hifadhi zao za dharura ili kukabiliana na hali ya uhaba wa mafuta uliojitokeza kufuatia mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.

IEA ni shirika la kiserikali lililoanzishwa mwaka wa 1974, ambalo hutoa mapendekezo ya sera, uchambuzi na data kuhusu sekta ya nishati duniani.

Nchi 32 wanachama na nchi 13 za jumuiya ya IEA zinawakilisha 75% ya mahitaji ya nishati duniani.

Uamuzi wa kuchukua hatua za pamoja za dharura ulifanywa kufuatia mkutano usio wa kawaida wa serikali wanachama wa IEA, ulioitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa IEA kutathmini hali ya soko huku kukiwa na mzozo wa Mashariki ya Kati na kuzingatia chaguzi za kushughulikia usumbufu wa usambazaji.

"Changamoto za soko la mafuta tunazokabiliana nazo ni kubwa mno, kwa hivyo ninafuraha sana kwamba nchi Wanachama wa IEA zimejibu kwa hatua ya dharura ya pamoja ya ukubwa ambao haujawahi kushuhudiwa," Mkurugenzi Mtendaji wa IEA Fatih Birol alisema.

"Masoko ya mafuta ni ya kimataifa kwa hivyo mwitikio wa usumbufu mkubwa unahitaji kuwa wa kimataifa pia. Usalama wa nishati ndio jukumu la msingi la IEA, na ninafurahi kwamba Wanachama wa IEA wanaonesha mshikamano mkubwa katika kuchukua hatua madhubuti pamoja."

IEA inasema hisa za dharura zitapatikana sokoni kwa muda unaolingana na hali ya kitaifa ya kila nchi Wanachama na zitaongezewa hatua za dharura na baadhi ya nchi.

Wanachama wa IEA wana hifadhi ya dharura ya zaidi ya mapipa bilioni 1.2 ya mafuta, na mapipa milioni 600 zaidi yakiwa akiba yaliyoshikiliwa na seriklai husika kwa ajili ya matumizi yao wenyewe.

Katika historia ya IEA, hili ni toleo la sita la akiba lililoratibiwa tangu Shirika lilipoundwa mwaka wa 1974.

Hatua za awali za pamoja zilichukuliwa mwaka wa 1991, 2005, 2011, na mara mbili mwaka wa 2022.

Mzozo wa Mashariki ya Kati ulioanza tarehe 28 Februari 2026 umezuia mtiririko wa mafuta kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, na usafirishaji wa bidhaa ghafi na zilizosafishwa kwa sasa chini ya 10% ya viwango vya kabla ya migogoro.

Hii inawalazimu waendeshaji katika eneo lote kufunga au kupunguza kiasi kikubwa cha uzalishaji.

Wastani wa mapipa milioni 20 kwa siku ya mafuta ghafi na bidhaa za mafuta zikivuka Mlango-Bahari wa Hormuz mwaka wa 2025, au karibu 25% ya biashara ya mafuta ya baharini duniani.

CHANZO:TRT Swahili
Soma zaidi
Trump asema Marekani itatwaa urani ya Iran nyumbani kwa kutumia 'mashine kubwa za uchimbaji'
Makombora ya Urusi yashambulia Ukraine na kuua watu 16
Iran yapendekeza miaka 5 ya kusitisha urutubishaji wa Uranium huku Marekani ikishinikiza miaka 20
Meli ya China iliowekewa vikwazo na Marekani yapita Mlango Bahari wa Hormuz
Zaidi ya theluthi moja ya miundombinu ya nishati Mashariki ya Kati imeathiriwa na vita vya Iran
Gazeti la Uingereza la The Daily Telegraph lafuta habari isiyo sahihi kuhusu Erdogan
Trump afikiria kuishambulia upya Iran baada ya mazungumzo ya amani ya Islamabad kushindikana-ripoti
Trump aagiza jeshi la Marekani kukamata meli yoyote inayolipa kuvuka mlango bahari wa Hormuz
Takriban watu 30 wamefariki katika mkanyagano kwenye ngome ya kihistoria ya Laferriere nchini Haiti
Hakuna makubaliano ya Marekani-Iran baada ya mazungumzo ya saa 21 nchini Pakistan, asema Vance
Marekani yakubali kuachilia mali ya Iran iliyozuiliwa ili kuendeleza mazungumzo ya Islamabad
Makamu wa Rais Vance awasili Pakistan kuanza mazungumzo muhimu ya Marekani na Iran
Korea Kaskazini, China zakutana, kukuza ushirikiano wa kimkakati
Rais Macron, Papa Leo wa 14 wajadili hali ya Mashariki ya Kati
Netanyahu asema Israel itaishambulia Hezbollah pale inapobidi
Kocha wa zamani wa Romania Mircea Lucescu afariki dunia
Bilionea Bill Gates kutoa ushahidi wake kuhusu faili za Jeffrey Epstein
Netanyahu: Tumeshambulia reli na madaraja ya Iran
Mbunge wa Marekani aanza mchakato wa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Waziri wa Ulinzi
Misri, Uturuki na Pakistan katika jitihada za upatanishi: Vyombo vya habari Marekani