| Swahili
AFRIKA
4 dk kusoma
Aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei azikwa, huku waombolezaji waapa kulipiza kisasi
Mamilioni ya watu wamekusanyika katika mji wa Mashhad kwa swala ya maiti iliongozwa na mtoto mkubwa wa Khamenei, Hojjatoleslam Seyyed Mostafa Hosseini Khamenei, kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA.
Aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei azikwa, huku waombolezaji waapa kulipiza kisasi
Khamenei alizikwa pamoja na mjukuu wake mchanga wa kike, mkwe wake, binti yake na mke wa Mojtaba Khamenei, Zahra Haddad Adel. /

Aliyekuwa kiongozi wa Iran, Ali Khamenei, amezikwa katika mji wake wa kuzaliwa wa Mashhad. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, waombolezaji waliohudhuria mazishi hayo, wametoa wito wa kutaka kulipiziwa kisasi kufuatia kuuawa kwake katika shambulio la pamoja la Marekani na Israel mwezi Februari. Pia walionesha msimamo mkali wa kupinga maelewano yoyote na maadui wa Iran.

Msafara wa mazishi ulimalizika saa 4:00 usiku wa Alhamisi katika Kaburi la Imam Reza, ambako mamilioni ya watu walishiriki sala za mwisho za kumuaga marehemu.

Wakati wa msafara huo, waombolezaji wametoa kauli wakipaza sauti kauli kama "Kifo kwa Marekani," "Kifo kwa Israel," na "Kifo kwa wapinzani wa Velayat-e Faqih (Utawala wa Mwanazuoni wa Kiislamu)." Pia walipeperusha bendera nyekundu, ambazo ni alama ya kutaka kulipiza kisasi, pamoja na bendera ya taifa la Iran.

Kwa mujibu wa IRNA, Khamenei alizikwa pamoja na mjukuu wake mchanga wa kike, mkwe wake, binti yake na Zahra Haddad Adel, mke wa Mojtaba Khamenei, ambao wote waliuawa katika shambulio la Marekani na Israel lililotokea Februari 28, siku ya kwanza ya vita kati ya Iran na muungano huo.

Mashambulizi hayo pia yameuwa viongozi wengi wa juu wa jeshi la Iran pamoja na takribani wanafunzi wadogo 160.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa Iran ilijibu mashambulizi hayo kwa kudhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu inayopitisha karibu asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa duniani kwa njia ya bahari, pamoja na kurusha makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya mataifa ya Ghuba yanayoshirikiana na Marekani, hatua iliyotikisa taswira ya utulivu wa nchi hizo zenye utajiri wa mafuta.

Waombolezaji walionekana wakijipiga vifua na kulia huku wakisubiri jeneza la Khamenei lifike katika Kaburi la Imam Reza, eneo takatifu zaidi kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iran na mahali ambapo marehemu alikuwa ameomba azikwe kwa mujibu wa wosia wake.

Helikopta ilitumika kulisafirisha jeneza katika sehemu ya mwisho ya safari kutokana na matarajio ya msongamano mkubwa wa watu.

Kutokana na kuibuka tena kwa mvutano kati ya Iran na Marekani, hata baada ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofanikishwa na Pakistan mwezi uliopita, ndege moja ya kivita ililisindikiza ndege iliyobeba mwili wa Khamenei kuelekea Mashhad.

Mazishi hayo yalihitimisha siku sita za shughuli za maombolezo zilizofanyika Tehran, Qom na pia Iraq, ambapo wananchi walipata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

Wachambuzi walifuatilia kwa karibu iwapo mrithi wa Khamenei, Mojtaba Khamenei, angejitokeza hadharani. Hata hivyo, hakuhudhuria ibada ya mazishi, huku ikidaiwa kuwa alijeruhiwa katika shambulio hilo lililomuua baba yake na baadhi ya wanafamilia wengine.

"Ni kisasi pekee kitakachopunguza maumivu"

Wanaume wengi walivaa mavazi meusi na wanawake walivaa buibui nyeusi na wengi wao wakipeperusha bendera nyekundu zinazowakilisha wito wa kulipiza kisasi.

Waombolezaji, walipaza kauli za kupinga maelewano na kumshambulia kwa maneno Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Kwa mujibu wa waandishi wa AFP, baadhi yao walibeba bango kubwa lililoandikwa kwa Kiingereza: "Hey Trump, we will kill you" (Trump, tutakuua).

Hoda, mwanamke mwenye umri wa miaka 35 aliyeshiriki mazishi hayo, alisema: "Kupoteza kiongozi wetu ni uchungu mkubwa kuliko hata kumpoteza mzazi. Ni kifo cha Trump na Netanyahu pekee kitakachopunguza maumivu yetu. Hakupaswi kuwa na maelewano yoyote."

Tangu alfajiri, maelfu ya waombolezaji waliovalia mavazi meusi walielekea kwenye Kaburi hilo huku wakibeba bendera nyekundu licha ya joto lililokaribia nyuzi joto 40.

Mohammad Afsharian, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 41, alisema: "Watu wote hapa wanataka kisasi. Sijui kuhusu diplomasia wala sera ya kuendelea na mazungumzo, lakini kila mtu amebeba bendera nyekundu kama ishara ya kutaka kulipiza kisasi." 

Hasira hizo zimeakisi ukosoaji kutoka kwa wenye misimamo mikali nchini Iran dhidi ya serikali ya Rais Masoud Pezeshkian, ambayo imekuwa ikikosolewa kwa kuendelea na mazungumzo na Marekani baada ya kuuawa kwa Khamenei.

Tahereh Rahmani, mwenye umri wa miaka 37 na msimamizi wa shule, alisema: "Ni kisasi pekee kitakachopunguza maumivu yetu. Tuko hapa na bendera zetu nyekundu kuomba kisasi kwa ajili ya kiongozi wetu." 

"Kutakuwa na umwagaji damu"

Karibu na kaburi la Imam Reza, watoto wengi walihudhuria mazishi hayo wakiwa pamoja na familia zao, wengi wao wakiwa wamevaa kofia zenye rangi za bendera ya Iran.

Karibu na hoteli inayoitwa Miami, bango kubwa lilikuwa na sura ya Donald Trump pamoja na tangazo la zawadi kwa yeyote atakayemuua.

Bango jingine lilikuwa na picha ya Benjamin Netanyahu likiwa na ujumbe wa Kiingereza uliosomeka: "There will be blood" — "Kutakuwa na umwagaji wa damu."

 

CHANZO:TRT World and Agencies