Uturuki na Italia huenda zikaandaa Kombe la Mataifa bora UEFA 2032

Kamati ya Utekelezaji ya UEFA itazifahamisha Uturuki na Italia iwapo zabuni yao ya kuandaa EURO 2032 kwa pamoja kwenye mkutano wake huko Nyon tarehe 10 Oktoba.

By Nuri Aden
Kamati ya Utekelezaji ya UEFA kuzifahamisha Uturuki na Italia iwapo zabuni yao ya kuandaa EURO 2032 kwenye mkutano wake huko Nyon tarehe 10 Oktoba. Picha: UEFA / Others

Matumaini ya mataifa ya Italia na Uturuki ya kuwa wenyeji wa pamoja wa dimba la UEFA EURO 2032, yamepigwa jeki baada ya uongozi wa Shirikisho la Soka Ulaya UEFA kuyafahamisha mataifa hayo kuwa itaamua wiki ijayo.

Wakati huo huo, Shirikisho la Soka la Uturuki limeondoa zabuni yake ya kuandaa Shindano la UEFA EURO 2028 kufuatia ombi jipya la zabuni ya pamoja na Italia.

Shirikisho la soka la Italia (FIGC) na shirikisho la soka la Uturuki (TFF) yameomba kuunganisha zabuni zao binafsi na kuwasilisha zabuni moja ya pamoja ya kuwa wenyeji wa dimba la UEFA EURO 2032.

Hapo mwanzoni, Shirikisho la Kandanda la Uturuki TFF liliingia katika mchakato wa zabuni ya Euro 2028 na EURO 2032, ilihali Shirikisho la Kandanda la Italia Figc, liliamua kuwasilisha zabuni tu kwa ajili ya toleo la 2032.

Zabuni hiyo ya pamoja imeitimiza mahitaji ya kuwasilishwa kwa kamati ya utendaji ya UEFA baada ya kufuata mahitaji, na itakaguliwa katika mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 10 Oktoba, ambapo uamuzi wa wenyeji wa makala ya EURO 2028 na EURO 2032 utafanywa.

Aidha, mashirikisho matano yakiwemo England, Ireland ya Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Scotland na Wales yamewasilisha zabuni ya pamoja ya kuandaa toleo la 2028 ya EURO.