Uturuki kuwa na miradi 'madhubuti' na Ethiopia katika umeme na nishati

Waziri wa Nishati anasema lengo ni kuimarisha ushirikiano katika uzalishaji wa umeme, miundombinu ya gridi ya taifa, uwekezaji katika nishati ya ukarabati na miradi ya umeme wa maji.

By
Rais wa Uturuki Erdogan na Waziri Mkuu Abiy wakishuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Uturuki na Ethiopia. /AA / AA

Uturuki imedhamiria kuimarisha ushirikishaji wa uzoefu katika sekta ya nishati na Ethiopia, kuanzisha miradi, na kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali, amesema Waziri wa Uturuki wa Nishati na Mali Asili, Alparslan Bayraktar siku ya Jumanne.

Makubaliano kati ya nchi hizo mbili katika ushirikiano wa nishati kati ya Wizara ya Uturuki ya Nishati na Mali Asili na Wizara ya Ethiopia ya Maji na Nishati yalisainiwa kati ya Bayraktar na Waziri wa Maji na Nishati Habtamu Itefa siku ya Jumanne wakati wa ziara ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan nchini Ethiopia.

Kupitia makubaliano hayo, nchi mbili hizo zitaendeleza miradi ya pamoja katika sekta ya uzalishaji umeme, nishati mbadala, na upatikanaji wa nishati, na kushirikiana katika uzalishaji na usimikaji wa vifaa vya uzalishaji umeme, na mitambo ya umeme.

Uwekezaji wa miundombinu ya umeme katika sekta binafsi na umma, hasa uzalishaji wa nishati ya umeme, na usambazaji, utaendelezwa, pamoja na kushirikiana katika kubadilishana taarifa na uzoefu kati ya taasisi husika.

"Tuna lengo la kuimarisha na kushirikiana katika uzoefu na kuzalisha miradi katika sekta mbalimbali, kuanzia uzalishaji wa umeme mpaka miundombinu ya gridi ya taifa, kuanzia uwekezaji katika nishati mbadala mpaka miradi ya miundombinu ya uzalishaji wa umeme wa maji," aliandika Bayraktar katika mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal.

"Tumekubaliana kudumisha ushirikiano wetu katika kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali, kuanzia nishati na madini, elimu, afya, usafiri, kilimo, mazingira, mipango miji, utamaduni, na utalii," ameongeza.