Mshambuliaji hatari Erling Haaland
Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland akiwa na kocha Pep Guardiola. / Reuters
Mshambuliaji hatari Erling Haaland
Ni mshambuliaji wa klabu ya Ligi Kuu ya England na timu ya taifa ya Norway.

Erling Braut Haaland ana umri wa miaka 25 na anaaminika kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani.

Anafahamika zaidi kwa kasi na uwezo wake na umalizaji wake akiwa kwenye eneo la 18.

Alianza kusakata soka akiwa na vilabu vya Norway kabla kujiunga na Red Bull Salzburg 2019.

Huko alishinda Ligi ya Bundesliga ya Austria na taji lingine nchini humo.

2020 akajiunga na Bundesliga ya Ujerumani Borussia Dortmund, miaka miwili baadaye akatua pale Manchester City.

Huko ndiko kumekuwa kama nyumbani kwake. Msimu wa kwanza tu akaonesha ya kwake, siyo kushinda mataji tu, bali aliweka rekodi ya mfungaji bora mwenye magoli mengi zaidi katika Ligi Kuu ya England msimu mmoja. Akicheka na nyavu mara 36.

Na katika tuzo za Ballon d’Or akamaliza wa pili.

Haaland kwa Man City amekuwa sehemu ya mafanikio makubwa kwa timu na yeye binafsi kujizolea sifa kede kede.

Ni mchezaji pekee kupata tuzo ya mchezaji bora kinda wa EPL na mchezaji bora wa msimu katika msimu mmoja.

Na ukitaka kujua kuwa ni mashine ya magoli, pia ni mchezaji wa kwanza aliyefunga ‘hat trick’ nane kwa haraka zaidi.

Erling Haaland alizaliwa Leeds, Uingereza wakati baba yake Alfie akiwa mchezaji wa Leeds United wakati huo.

Na bado akiwa imara na makali yake, je, Erling Halaand atafanikiwa kuipa Manchester City mataji zaidi?

CHANZO:TRT Afrika Swahili