Rais wa Uturuki ateuwa Waziri mpya wa Katiba na Mambo ya Ndani katika mabadiliko ya Baraza la Mawazi
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Istanbul Akin Gurlek ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba, huku Gavana wa Erzurum Mustafa Ciftci akichukua Wizara ya Mambo ya Ndani.
Uturuki imeteuwa mawaziri wapya wa Katiba na Mambo ya Ndani kufuatia amri ya rais iliyosainiwa na Rais Recep Tayyip Erdogan na kuchapishwa katika gazeti la serikali.
Kwa mujibu wa amri hiyo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Istanbul Akin Gurlek ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba, akichukua nafasi ya Yilmaz Tunc, huku Gavana wa Erzurum Mustafa Ciftci akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Ali Yerlikaya.
Uteuzi huo umefanyika nchini ya kifungu 104 na 106 cha Katiba ya Uturuki.
Kufuatia tangazo hilo, Ali Yerlikaya amethibitisha kupokezana majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Mustafa Ciftci na kumtakia kila la kheri katika uteuzi wake.
Katika taarifa iliyowekwa katika mtandao wa kijamii, Yerlikaya amesema alitumikia Wizara ya Mambo ya Ndani tangu Juni 4, 2023, kwa uthibitisho wa Rais Erdogan, na kuonesha shukrani zake kwa msaada alioupata kutoka kwa Rais katika kipindi chake kama waziri.
Pia amewashukuru watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa utumishi wao kwa kuhakikisha usalama na ulinzi wa umma, na kumalizia ujumbe wake kwa kumtakia kila la kheri aliyemrithi.
Yilmaz Tunc nae hivyo hivyo alitoa ujumbe wa kuaga baada ya uteuzi wa Akin Gurlek kama Waziri wa Katiba.
Tunc amesema kufanya kazi na Rais Erdogan na kuchangia safari ya kisiasa ya chama tawala imekuwa ni fahari kubwa, na kusema kuwa uteuzi wake kama Waziri wa Katiba Juni 2023, ulikuwa na majukumu makubwa.
Alionesha mabadiliko yaliyofanyika katika kipindi cha miaka 23 chini ya uongozi wa Erdogan kwa kukuza demokrasia na sheria, na kuongeza kwamba ataendelea kutumikia nchi katika siku zijazo kwenye majukumu mengine.
Tunc pia amempongeza Gurlek na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya.
Uteuzi huo unafanyika mara moja baada ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.