Waziri Mkuu wa Libya afanya mabadiliko ya serikalini kwa lengo la kuimarisha utoaji huduma

Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh amefanya mabadiliko katika serikali, akisema siku ya Alhamisi kuwa anataka kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi.

By
Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh amefanya mabadiliko ya serikali yake Machi 12, 2026. / TRT Afrika

Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh amefanya mabadiliko katika serikali, akisema siku ya Alhamisi kuwa anataka kuimarisha utoaji huduma.

Dbeibeh ataendelea kuwa waziri wa ulinzi na waziri wa mambo ya nje, lakini amelenga kuondoa tofauti za kikanda katika baraza jipya la mawaziri huku 10 kati ya mawaziri 27 wakibadilishwa.

Lengo la mabadiliko hayo ni ‘‘kuimarisha utoaji huduma wa serikali’’, kulingana na mtandao wa serikali wa Hakomitna.

‘‘Lengo siyo kubadilisha tu, lakini kuimarisha utoaji huduma kwa raia’’, Dbeibeh alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii.