| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Wakenya kulipia zaidi umeme baada ya gharama kupanda
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli, EPRA imetangaza ongezeko la asilimia 8.7 ya malipo ya nishati umeme.
Wakenya kulipia zaidi umeme baada ya gharama kupanda
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya,EPRA imetangaza ongezeko la 8.7% ya malipo ya nishati. / Picha: Reuters / Reuters
11 Januari 2024

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya,EPRA imetangaza ongezeko la 8.7% ya malipo ya nishati.

" Ina maana kwamba kaya za Kenya zitalipa hadi 16.5% zaidi ya umeme mwezi huu," mtaalamu wa kiuchumi @mwangocapital imesema katika mtandao wa X,

"Hili ni pigo kubwa kwa watumiaji ambao tayari wanatatizika na kupanda kwa gharama ya maisha," imeongezea.

Shirika la EPRA limeongeza bei ya mafuta na ya fedha za kigeni kwenye bidhaa hiyo, na hiyo itaongeza bei ya umeme.

Bei ya kila unit ya umeme sasa itamgharimu mkenya 0.027 ya dola ambayo ni sawa na shilingi 4.33 za Kenya kwa 0.025 dola (shilingi 3.93) kwa kila unit.

Shirika la EPRA pia iliongeza marekebisho ya kupanda kwa thamani ya fedha za kigeni kwa 103.7% hadi dola 0.040 kutoka dola 0.020 mwezi uliopita.

" Ongezeko la 16% la tokeni kwa @KenyaPower ni mzigo wa hivi punde usiokubalika kwa Wakenya waliochoka, wenye njaa na wenye hasira," Kalonzo Musyoka mwanasisas ana mwenyekiti wa Chama cha Wiper amesema ,

Kalonzo alikuwa katika kamati ambayo iliundwa na upande wa upinzani kujadili na seriklai ya William Ruto malalamishi ya wananchi mkiwemo hgharama ya juu ya maisha.

" Huu ni mfano wa Serikali ya Kenya Kwanza kutokuwa na uwezo wa kushughulikia gharama ya maisha. Wanataka kutuacha gizani, lakini nawaambia, mjue kuna nuru gizani," ameongezea katika mtandao wa X.

Kenya Kwanza ni chama cha rais William Ruto.

CHANZO:TRT Afrika