tokea masaa 3
Watoto wadogo wanne wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa kwa visu katika shule mmoja jijini Kampala, Uganda.
“Tunathibitisha kutokea kwa tukio hilo katika shule ya awali ya Ggaba katika eneo la Makindye ambapo mtuhumiwa mmoja aliwashambulia watoto wanne wadogo kwa kuwachoma na kisu,” alisema msemaji wa polisi wa eneo la Kawaala, Kawala Racheal kupitia taarifa yake.
Kulingana na msemaji huyo, jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi kufuatia tukio hilo, likiwa linamshikilia mtu mmoja hadi sasa.
Inadaiwa kuwa, mtuhumiwa huyo alijifanya kuwa mzazi kwa mmoja wa wanafunzi shuleni hapo, na kuingia ndani ya eneo la shule na kuwashambulia watoto hao.
Waliouawa ni watoto wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka mitatu na minne.













