Bosi wa Shirikisho la Soka nchini Congo matatani kwa utakatishaji fedha za FIFA
Wapelelezi katika kesi hiyo, wanadai kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zilipelekwa kwenye matumizi binafsi ya Mayolas.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Congo (FECOFOOT) Jean-Guy Blaise Mayolas amepewa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji wa fedha zenye thamani ya Dola milioni 1.3 zilizotolewa na FIFA.
Mayolas amekutwa na hatia hiyo, pamoja na mkewe na mtoto wake.
Fedha hizo, ambazo zilikuwa sehemu ya ruzuku wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19, zilikuwa zitumike kwenye miradi ya kuendeleza mchezo wa soka nchini Congo, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa michezo na kukuza soka la wanawake nchini humo.
Inadaiwa kuwa, FECOFOOT ilipokea Dola 20,000 kati ya zile zilitengwa na FIFA, kama ruzuku kwa nchi wanachama wakati wa kupambana na ugonjwa wa Uviko-19.
Wapelelezi katika kesi hiyo, wanadai kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zilipelekwa kwenye matumizi binafsi ya Mayolas.