Ali Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Tanzania afariki
Kifo cha Mzee Ali Hassan Mwinyi kimetokea katika Hospitali ya Mzena, Dar es salaam, Tanzania, na amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 98.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amelihutubia taifa kutoka Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam Ahamisi na kutoa taarifa ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amefariki katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam.
Mwinyi, alikuwa rais wa awamu ya pili wa taifa Hilo la Afrika Mashariki kuanzia mwaka 1985 hadi 1995.
Rais huyo wa zamani pia aliwahi kushikilia nyadhifa mbalimbali za mawaziri, ikiwa ni pamoja na mambo ya Ndani, Afya na Rasilimali za asili.
Mzee Mwinyi alichaguliwa kuwa mrithi wake na Baba wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alipostaafu mnamo Oktoba 1985.
Soma zaidi kuhusu
Safari ya Rais Mwinyi kupitia link hii hapa
Safari ya Mzee Mwinyi; Urais ambao hakuutegemea