Upigaji kura wa serikali za mitaa waanza Uturuki
Katika mikoa ya mashariki mwa nchi, upigaji kura umeanza saa moja asubuhi huku maeneo mengine ya Uturuki, vituo vimefunguliwa saa baadae.
Kura zimeanza kupigwa nchini Uturuki siku ya Jumapili kuchagua mameya wa majiji, mameya wa wilaya na viongozi wengine wa serikali za mitaa ambao watakuwa madarakani kwa miaka mitano ijayo, ikiwemo katika majiji yenye ushindani mkali ya Istanbul, Ankara na Izmir.
Kura zimeanza kupigwa saa moja asubuhi kwa saa za Uturuki na zitaendelea mpaka saa kumi jioni katika mikoa 32 ya mashariki, na mikoa iliyobaki, vituo vimefunguliwa saa mbili asubuhi na vitafungwa saa kumi na moja jioni.
Katika uchaguzi wa Machi 31, zaidi ya wapiga kura milioni 61 nchi nzima watawe kupiga kura zao katika vituo vya kupiga kura zaidi ya 200,000, huku wagombea wakitoka katika vyama vya siasa 34.
Vyama vikuu vinavyotoana jasho ni pamoja na chama tawala cha Justice and Development (AK) Party, chama kikuu cha upinzania Republican People's Party (CHP), pamoja na Nationalist Movement Party (MHP), Good (IYI) Party, na chama cha Peoples' Democratic Party (DEM Party).
Wapiga kura wanaruhusiwa kupiga kura wagombea wao katika wilaya zao. Kuna wapiga vijana milioni 1.32 wanaopiga kura kwa mara ya kwanza.
Jiji la Istanbul, kiti cha Utawala wa Ottoman, lina wagombea 49.
Zaidi ya masanduku 1,000 ya kupiga kura yamewekwa kwa wale ambao hawataweza kwenda katika vituo vya kupiga kura kwa sababu ya ugonjwa au ulemavu.
Siku ya uchaguzi, uuzaji na unywaji wa vinywaji vya ulevi hautaruhusiwa katika maeneo yote yanayotoa huduma hiyo na maeneo ya umma kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa sita usiku.
Vituo vya redio na television haviruhusiwa kufanya matangazo, kubashiri au kuzungumzia kuhusu uchaguzi au matokeo ya uchaguzi mpaka saa kumi na mbili jioni.
Kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tatu usiku, matangazo yanayohusiana na uchaguzi yanatakuwa kutumia matangazo au habari kutoka kwa Baraza Kuu la Uchaguzi (YSK).