Katika Picha: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Uturuki, waashiria ukomavu wa demokrasia ya taifa

Raia wa Uturuki wanashiriki katika mchakato wa kidemokrasia kwa namna pekee  sana, kutoka kwa wazee wanaopiga kura zao katika vituo vya kupigia kura ndani ya nyumba za wazee hadi wapiga kura waliovalia  kitamaduni.

By trtafrikaswa
Mchakato wa upigaji kura utaendelea mpaka saa 10 jioni katika majimbo 32 ya upande wa Mashariki, wakati katika maeneo mengine, vituo vya upigaji kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 11 jioni/ Picha:  AA   / Others

Mamilioni ya raia wamepanga foleni katika vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utaamua hatma ya wagombea 1000 katika majimbo 32 nchini.

Wakiwa wamevalia nandifu, watu wengi walijitokeza katika vituo zaidi ya 200,000 kuchagua wagombea wanaowataka kutoka vya vya siasa 34 vinavyoshiriki uchaguzi huo. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Edodogan walipiga kura zao mjini Istanbul.

Hizi ni baadhi ya taswira za mchakato huo.

Katika eneo la Sakarya, mpiga kura asiyejiweza alipiga kura yake nyumbani, kupitia masanduku yanayohamishika yaliyotolewa na Baraza Kuu la Uturuki la Uturuki (YSK).

Masanduku ya kura yaliingizwa kwenye nyumba za wagonjwa na kisha kuwekwa kwenye magari.

Kituo cha kupigia kura kiliwekwa katika nyumba ya kutunzia wazee katika eneo la Duzce. Watu wanaotumia baiskeli maalumu na fimbo walianza kupiga kura mara baada ya kuanza kwa zoezi hilo.

Katika kituo cha Ankara, wakazi kutoka kituo cha matunzo na urekebishaji walishiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Uturuki.

Watu kutoka jamii ya Kyrgyz waishio katika wilaya ya Ercis district ya Van wlaivalia mavazi yao ya kitamaduni huku wakielekea katika masunduku ya kupigia kura katika shule ya msingi ya Ulupamir.

Msanii Bülent Akay, ambaye ameshiriki nafasi ya "Hacivat" katika matukio ya ndani ya nchi na ya kimataifa na kupewa heshima na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya Uturuki, alifika kwenye kituo cha kupigia kura akiwa amevaa mavazi yake.

Chanzo: TRT World na Mashirika