| swahili
AFRIKA
7 DK KUSOMA
Afrika Kusini: Miaka 30 baadaye
Licha ya mtazamo wa jumla, wakosoaji wanakubali kwamba kumekuwa na juhudi za makusudi kutoka kwa serikali mbalimbali ili kuinua nchi kutoka kwa umaskini na hasa kwa kuwekeza kwa watu wake.
Afrika Kusini: Miaka 30 baadaye
Licha ya juhudi nyingi katika kukuza  elimu, na hatua za kuondoa ubaguzi, Waafrika Kusini Weusi wanaonekana kuwa nyuma katika masomo,/ Picha : Reuters 
8 Mei 2024

Na Dayo Yussuf

‘’Afrika Kusini bado hatuna jina mpaka leo. Kwa sababu Afrika Kusini sio jina, ni mwelekeo, Kusini mwa Afrika, sio jina. Tunahitaji jina kwa nchi hii.’’

Alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mwaka wa 2021, Julius Malema alizungumzi akwa hisia nyingi jina la nchi yake.

Akiwa rais wa chama cha Economic Freedom Fighters nchini Afrika Kusini, na amehudumu kama mbunge kwa muongo mmoja, ni mwanasiasa ambaye watu humsikiliza anapozungumza.

Na anajua hili na mara nyingi kauli zake zinasukuma mabadiliko, kisiasa.

Lakini miaka 30 tangu uhuru wake, je, ni haki kuwa kuwa bado hii ndiyo mada ya mjadala katika nchi iliyoendelea sana sio kisiasa tu bali pia inayochukuliwa kuwa gwiji wa uchumi katika bara hili?

Lakini unapotaka kuangalia nyuma ukuaji wa nchi nadhani inaleta maana kwenda tangu mwanzo.

Uwekezaji katika watu wake

Licha ya mtazamo wa jumla, wakosoaji wanakubali kwamba kumekuwa na juhudi za makusudi kutoka kwa serikali mbalimbali ili kuinua nchi kutoka kwa umaskini na hasa kwa kuwekeza kwa watu wake.

''Uwekezaji muhimu katika elimu umekuwa uanzishwaji wa Shule za Utaalam, ambazo ni za kwanza za aina yake nchini,'' anasema Aluwani Chokoe, Msemaji wa Baraza la Vijana la ICT, taasisi isiyo ya kiserikali inayotetea ushirikishwaji wa vijana kiuchumi.

‘’Shule hizi zinakwenda zaidi ya mtaala wa kawaida wa Shule za Kawaida za Umma, unaowezesha wanafunzi kubobea katika Hisabati, Sayansi na Teknolojia, Uhandisi; Biashara na Ujasiriamali, Michezo na Sanaa ya Maonyesho na Ubunifu,’’ Aluwani anaiambia TRT Afrika.

Licha ya juhudi hizi katika elimu, na hatua za kuondoa ubaguzi, Waafrika Kusini Weusi wanaonekana kuwa nyuma katika masomo, jambo ambao baada ya muda mrefu limeaathiri upatikanaji wa ajira kwao.

‘’Vijana wanapigania kupata elimu na fursa ili kuboresha maisha yao na hili ndilo ambalo serikali imekuwa ikiendelea na sera na mipango yake yote katika kipindi cha miaka thelathini iliyopita,’’ anasema Aluwani.

Ukuaji wa uchumi

Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, uchumi wa Afrika Kusini umeona ukuaji mkubwa hasa kutokana na kumalizika kwa ubaguzi wa rangi na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa.

Benki ya Dunia inakadiria kuwa Pato la Taifa la nchi lilipanda kutoka $153bn mwaka 1994 hadi $458bn mwaka 2011, katika miaka 10 tu ya kwanza.

Mwenendo ulisalia mwendo kwa miaka mingi, ingawa polepole ulipunguza kasi ya kulungu kwa mambo mengine yanayojitokeza.

Wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi mwaka huu, vijana wanataka kuona mabadiliko makubwa ya kuirejesha nchi kwenye mstari wa uhuru wa kiuchumi.

''Ripoti ya hivi majuzi ya PWC (Aprili 2024) imegundua kuwa licha ya changamoto nyingi ambazo nchi yetu inakabili, uchumi wetu ulivutia takriban bilioni 100 katika uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) mwaka 2023, sawa na 1.4% ya Pato la Taifa,'' inaendelea. kueleza ALuwani.

‘’Tunataka kuona kusitishwa kwa kuzorota kwa utoaji huduma katika vitongoji na makazi holela katika miji mikuu katika miungano. Ukosefu wa ajira na uhalifu. Waafrika Kusini wanataka jamii inayostawi ya kidemokrasia na taifa lenye uwezo wa kimaendeleo,’’ anaongeza.

Ukosefu wa usawa na ubaguzi wa rangi

Lakini doa jeusi kutoka kwa siku zake za nyuma bado linasumbua hali ya sasa ya Afrika Kusini.

Licha ya ukuaji wa uchumi na ongezeko kubwa la Pato la Taifa la nchi, pato la taifa halijagawa kwa usawa kwa raia wote.

Wengi wa Waafrika Kusini Weusi bado wanapata sehemu ndogo ya keki ya kitaifa.

‘’Afŕika Kusini bado ni jamii isiyo na usawa zaidi ya kiuchumi duniani, ikishuhudiwa na mambo kadhaa. Hii ni licha ya sera zilizowekwa na hatua ya uthibitisho. Bado kuna uwakilishi mdogo wa watu weusi waliopungukiwa katika historia katika viwango vya juu vya uchumi,’’ anasema Aluwani.

Aluwani anaamini kwamba daima kutakuwa na mtafaruku kati ya watu wa rangi tofauti mradi bado kuna baadhi ya watu wanaoamini kuwa wako bora kuwaliko wengine.

‘’Kuna wapinzani wa demokrasia ambao daima wanakataa kuwatambua Waafrika Kusini weusi kama washiriki sawa katika jamii na katika uchumi,’’ anasema. Lakini hii inazidi kutoweka.

Vizazi vichanga vina wasiwasi zaidi kuhusu mustakabali chanya wa Afrika Kusini kuliko kizazi kongwe zaidi ambacho bado kupona kutokana na majeraha ya siku zilizopita, na kama anavyosema Aluwani hili linahitaji kuainishwa kwa ajili ya ukuaji mkubwa zaidi.

''Katika kila jamii, kuna mizani ya ushindani kati ya mapambano na mafanikio ya kizazi kilichopita na ndoto na matarajio ya kizazi kijacho, na jamii zote zilizofanikiwa ni zile ambazo zimeweza kuweka mvutano huu kwa njia chanya kufikia malengo yao ya kimaendeleo.

Dari ya kizazi kilichopita inatakiwa kuwa msingi na jukwaa la kuruka la kizazi kijacho. Hii si hali ya kipekee kwa Afrika Kusini na ni jinsi tunavyoitumia ndiyo itaamua iwapo tutajenga taifa lenye umoja, lenye mafanikio, linaloshinda au la.’’

Ripoti ya hivi majuzi ya PWC imefanya ugunduzi kwamba licha ya changamoto nyingi ambazo Afŕika Kusini ilikabiliana nazo, uchumi ulivutia karibu dola bilioni 100 (dola Bilioni 5) katika uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) mwaka 2023, sawa na asilimia 1.4 ya Pato la Taifa.

Kwa mujibu wa Aluwani, hii ni taswira nzuri na imani iliyonayo nchi kwa wawekezaji wa kigeni.

‘’Takwimu zinaonyesha kuwa raia wa kigeni wana hisia ‘chanya kiasi’ kuhusu mazingira ya uwekezaji na biashara nchini na viwango vya utawala wa umma.’’

Kwa hivyo kufikia Mei 29, nchi itapiga kura kwa mara ya 7 kuchagua serikali ya kidemokrasia inayoakisi kile kinachojulikana kama taifa la upinde wa mvua, nchi ya wote kwa wote. Swali linabaki je, viongozi wajao wataipeleka nchi mbele zaidi au wataendelea kupambana na mashetani wa zamani na wa sasa?

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi
AU yakanusha tuhuma za Trump kuhusu mauaji ya halaiki Nigeria
Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu Tanzania
Jaji Mkenya achaguliwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amfuta kazi makamu wake
Duma wa Botswana aipa India zawadi ya duma 8
Kesi ya Roger Lumbala wa DRC yaanza kusikilizwa
Kesi za ubakaji, watoto kupotea zaripotiwa Darfur, Sudan – Umoja wa Mataifa
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukika
Libya yatakiwa kufunga vituo vya kuwazuilia wahamiaji katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
Rais Museveni aonya kuzuka kwa vita endapo nchi za Afrika zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32
Ghana yafichua sababu ya ajali ya helikopta iliyoua watu wanane, wakiwemo mawaziri, mwezi Agosti